-
Iran yakanusha madai kuwa imeishambulia UAE kwa makombora
Aug 19, 2026 04:18Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imekanusha vikali madai ya Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) kwamba Iran imevurumisha makombora mawili ya balestiki kuelekea nchi hiyo.
-
Iran yamtahadharisha Trump kuhusu 'fikra potofu' ya kudai Mlango-Bahari wa Hormuz ni eneo la Marekani
Aug 19, 2026 04:16Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran anayeshughulikia Masuala ya Kisheria na Kimataifa Kazem Gharibabadi amemkosoa vikali Rais Donald Trump wa Marekani kwa madai yake kuhusu Lango la Bahari la Hormuz, akionya kuwa "fikra yake potofu" ya kuihesabu njia hiyo muhimu ya maji kama "eneo jipya la Marekani" inapasa kurekebishwa, la sivyo Tehran itamweka sawa.
-
Nigeria inachunguza shambulio lililosababisha vifo vya watu 25 katika jimbo la Plateau
Aug 19, 2026 04:12Watu wasiopungua 25 wameuawa katika shambulio dhidi ya kijiji kimoja katika jimbo la Plateau katikati mwa Nigeria.
-
Sudan Kusini yazidisha jitahada za kukabiliana na Ebola katika mpaka wake na Kongo
Aug 19, 2026 04:11Sudan Kusini imeimarisha ufuatiliaji wa maambukizi ya Ebola katika mpaka wake na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, ambapo harakati kubwa za watu kuvuka mpaka na matumizi ya njia zisizo rasmi zinaleta changamoto.
-
Ripoti: Vikosi vya Yemen vyashambulia kiwanda cha kusafisha mafuta cha Saudia cha Aramco katika mji wa Jizan
Aug 19, 2026 04:08Vikosi vya ulinzi vya Yemen vimetekeleza kwa mafanikio mashambulizi dhidi ya kituo cha mafuta kinachoendeshwa na kampuni ya serikali ya mafuta na gesi asilia ya Saudi Arabia ya Aramco, ikiwa ni hatua ya kulipiza kisasi dhidi ya uchokozi na mzingiro unaoendelea kutekelezwa na utawala wa Riyadh dhidi ya Yemen.
-
Marasimu ya Arubaini ya kumuenzi Kiongozi shahidi wa Iran na familia yake yafanyika Musalla wa Imam Khomeini, Tehran
Aug 18, 2026 15:39Sambamba na kutimia siku arubaini tangu kufanyika mazishi ya kihistoria ya kiongozi wa Iran aliyeuliwa shahidi, shughuli ya kumbukumbu ya kumuenzi kiongozi huyo shahidi na familia yake imefanyika leo katika eneo la Swala (Mosalla) la Imam Khomeini (RA) mjini Tehran.
-
Pezeshkian: Ustahimilivu, umoja, na matumaini ni nguzo ya Iran kukabiliana na vitisho vya nje
Aug 18, 2026 11:43Rais wa Iran, Masoud Pezeshkian, amesema vita vya Iraq dhidi ya Iran, vinavyofahamika nchini Iran kama Vita vya Kujihami Kutakatifu, vina somo muhimu ambalo ni ustahimilivu, umoja, na matumaini.
-
Qalibaf: Iran italipiza kisasi damu ya Kiongozi Shahidi
Aug 18, 2026 11:41Spika wa Bunge la Iran, Mohammad Baqer Qalibaf, ameahidi kwamba Jamhuri ya Kiislamu haitaruhusu damu ya Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu aliyeuawa shahidi, Ayatollah Sayyid Ali Khamenei, na mashahidi wengine wa uvamizi wa Marekani na Israel dhidi ya taifa hili “kupotea bila kulipiziwa kisasi.”
-
Kamanda: Iran ilitungua ndege zaidi ya 200 za adui katika Uvamizi wa Marekani na Israel
Aug 18, 2026 11:38Naibu Mkuu wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) amesema kuwa mifumo ya ulinzi wa anga ya Iran ilitungua ndege za adui zaidi ya 200, zikiwemo ndege zisizo na rubani (drones) na ndege zenye marubani, wakati wa uvamizi wa hivi karibuni wa Marekani na Israel.
-
Lavrov: Wanajeshi wa Ukraine Wanahusika na Ugaidi dhidi ya Nchi za Afrika
Aug 18, 2026 11:37Waziri wa Mambo ya Nje wa Russia, Sergey Lavrov, amesema kuwa Moscow imetiwa wasiwasi na ripoti zinazoashiria kuwa wanajeshi wa Ukraine wanahusika katika operesheni zinazotekelezwa na makundi haramu ya wanamgambo dhidi ya nchi za ukanda wa Sahel barani Afrika.