-
Jerusalem Post: Israel imeshtushwa na kasi ya Iran ya kujiimarisha upya kijeshi
Aug 15, 2026 03:53Gazeti la kizayuni la Jerusalem Post limefichua kuwa, maafisa wa ulinzi wa Israel wameshtushwa na namna Iran ilivyojenga upya na kwa kasi uwezo wake wa kijeshi tangu baada ya mashambulizi makali ya Marekani na utawala huo wa kizayuni wakati wa kipindi cha mwanzoni mwa vita vya kichokozi vilivyoanzishwa na tawala mbili hizo dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu.
-
Uturuki yaitaka Tunisia imuachie kiongozi wa chama cha Kiislamu cha Ennahda anayesota gerezani
Aug 15, 2026 03:51Spika wa Bunge la Uturuki, Numan Kurtulmus, ametoa wito wa kutaka kiongozi wa chama cha Kiislamu cha Ennahda na Spika wa zamani wa Bunge la Tunisia, Rached Ghannouchi, ambaye anaendelea kusota gerezani, apatiwe matibabu na kuachiwa kwa kuzingatiwa utu na ubinadamu.
-
Zaidi ya 70% ya Wapalestina wanapinga HAMAS kukabidhi silaha kabla Israel kuondoka kikamilifu Ghaza
Aug 15, 2026 03:49Uchunguzi mpya wa maoni uliofanywa na Kituo cha Utafiti wa Sera na Utafiti cha Palestina (Palestinian Center for Policy and Survey Research) unaonyesha kuwa, zaidi ya asilimia 70 ya Wapalestina wanapinga Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Palestina, HAMAS kukabidhi silaha zake kabla utawala wa kizayuni wa Israel kuondoka kikamilifu katika Ukanda wa Ghaza.
-
Israel imebomoa kikamilifu misikiti 1,076 Ghaza, imeharibu 165 na kubakisha 34 tu
Aug 15, 2026 03:40Wizara ya Wakfu na Masuala ya Kidini ya Ghaza imetangaza kuwa, kati ya jumla ya misikiti 1,275 ya eneo hilo la Palestina inayokaliwa kwa mabavu, 1,076 imebomolewa kikamilifu, 165 imebomolewa baadhi ya sehemu, na misikiti 34 pekee ndiyo iliyosalimika na jinai za jeshi la utawala wa kizayuni wa Israel.
-
Ayatullah Khatami: Uwezo wa makombora wa Iran umeidhalilisha Marekani
Aug 14, 2026 10:11Khatibu wa Sala ya Ijumaa iliyosaliwa leo hapa mjini Tehran amesema kuwa, Marekani ilitaka kuangamiza uwezo wa makombora wa Iran, lakini ilishindwa na kuufeli katika mpango wake huo.
-
Tehran: Taarifa ya Ufaransa na washirika wake wa Magharibi dhidi ya Iran ni propaganda za kinafiki za kupotosha ukweli
Aug 14, 2026 10:09Kaimu Mkuu wa Idara ya Haki za Binadamu ya Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amelaani hatua ya Ufaransa na baadhi ya nchi za Magharibi ya kutoa taarifa ya pamoja dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kwa kisingizio cha masuala ya haki za binadamu na kusema kuwa hatua hiyo ni mfano wa wazi wa unafiki wa kupotosha uukweli wa mambo.
-
Abdul-Malik al-Houth: Kukaririwa vitendo vya kuivunjia heshima Qur’ani kumefichua zaidi uadui wa Wazayuni
Aug 14, 2026 10:08Kiongozi wa Harakati ya Ansarullah ya Yemen amesema, kukaririwa vitendo vya kuivunjia heshima Qur’ani Tukufu kumefichua kwa uwazi zaidi uadui wa Wazayuni dhidi ya misingi yote mitakatifu, pamoja na chuki yao dhidi ya ujumbe wa Mwenyezi Mungu.
-
Mlipuko wa Ebola Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo wasambaa hadi mkoa wa sita
Aug 14, 2026 10:06Mlipuko wa ugonjwa wa Ebola katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo umeenea hadi mkoa wa sita, baada ya kifo kimoja kurekodiwa katika mkoa wa Bas-Uele, ambao hapo awali haukuwa umeathiriwa na mlipuko huo.
-
Mali: Wanajeshi 82 waliotekwa nyara na makundi yenye silaha wameachiliwa huru
Aug 14, 2026 10:05Serikali ya Mali imetangaza kuwa wanajeshi wake 82 waliokuwa wametekwa nyara na makundi yenye silaha wameachiliwa huru.
-
Iran: Hakuna chombo kinachoweza kupita salama Hormuz bila idhini
Aug 14, 2026 03:31Msemaji wa Kamandi Kuu ya Majeshi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ijulikanayo kama Makao Makuu ya Khatam al-Anbiya amekanusha madai ya Marekani kwamba meli zinaendelea kupita kwa hali ya kawaida katika Lango Bahari la Hormuz, akisema hakuna chombo kinachoweza kuvuka kwa usalama njia hiyo ya kimkakati bila idhini na uangalizi wa Iran.