WHO: Hakuna mgonjwa mpya wa Ebola aliyerekodiwa Bulape DRC kwa siku 20
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i132142-who_hakuna_mgonjwa_mpya_wa_ebola_aliyerekodiwa_bulape_drc_kwa_siku_20
Ofisi ya Kanda ya Afrika ya Shirika la Afya Duniani (WHO) imetangaza kuwa, hakuna mgonjwa mpya wa Ebola aliyerekodiwa au kuthibitishwa kwa siku 20 katika kanda ya afya ya Bulape, iliyoloko katika mkoa wa Kasai katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, ambako ugonjwa huo umekuwa ukiendelea kwa zaidi ya mwezi mmoja.
(last modified 2025-10-18T13:24:59+00:00 )
Oct 18, 2025 13:24 UTC
  • WHO: Hakuna mgonjwa mpya wa Ebola aliyerekodiwa Bulape DRC kwa siku 20

Ofisi ya Kanda ya Afrika ya Shirika la Afya Duniani (WHO) imetangaza kuwa, hakuna mgonjwa mpya wa Ebola aliyerekodiwa au kuthibitishwa kwa siku 20 katika kanda ya afya ya Bulape, iliyoloko katika mkoa wa Kasai katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, ambako ugonjwa huo umekuwa ukiendelea kwa zaidi ya mwezi mmoja.

Tangazo hili linaashiria hatua ya kutia moyo katika mapambano dhidi ya mlipuko wa ugonjwa huuo. Kulingana na WHO, wagonjwa 18 wametangazwa kuwa wamepona na wameunganishwa na familia zao, huku mgonjwa mmoja tu akisalia chini ya uangalizi wa matibabu.

Viongozi wa mkoa huo wanatoa wito kwa wakaazi kuendelea kuwa waangalifu, kufuata hatua za kuzuia, na kuimarisha ufuatiliaji wa jamii ili kuzuia kutokea tena kwa virusi vya ugonjwa huo.

Shirika la Afya Duniani (WHO) lililitangaza mwanazonbi mwa mwezi huu kwamba, mlipuko wa ugonjwa wa Ebola kusini mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo unaonyesha "dalili za kupungua kwa maambukizi".

Tangu kuanza kwa mlipuko wa ugonjwa huuo, wanawake wanatajwa kuambukizwa pakubwa idadi ambayo ni sawa na 57.8%, huku watoto wenye umri wa kuanzia wa hadi miaka tisa wakiunda asilimia 25.

Ebola ni ugonjwa hatari unaosababishwa na virusi vinavyojulikana kitaalam kama (Ebola Virus). Ugonjwa huu ni miongoni mwa magonjwa yajulikanayo kwa ujumla kama Homa za virusi zinazosababisha kutoka damu sehemu za wazi za mwili mfano puani , masikioni na machoni. Ugonjwa huu unaathiri binadamu na wanyawa kama vile nyani , ngedere, sokwe na popo.