-
Abdulmalik al-Houthi: Magharibi inawatumia wakufurishaji kuchafua sura ya Uislamu
Oct 19, 2020 23:04Katibu Mkuu wa Harakati ya Ansarullah ya Yemen amesema Marekani, Ufaransa na nchi zingine za Magharibi ndio waungaji mkono wa mwanzo kabisa wa makundi ya ukufurishaji huko Syria, Yemen na katika nchi zingine za Kiislamu kwa sababu zinawatumia wakufurishaji hao kuchafua jina la dini tukufu ya Uislamu.
-
Serikali ya Yemen: Tunashikilia mateka maelfu ya mamluki wa Saudia na Sudan
Oct 18, 2020 00:55Kamati ya Taifa inayoshughulikia masuala ya matekani nchini Yemen imetangaza kuwa jeshi la nchi hiyo linawashikilia mateka maelfu ya askari mamluki na vibaraka raia wa Saudi Arabia na Sudan.
-
Mapitio ya sababu za kutokea Mapinduzi ya Yemen ya Septemba 21
Sep 23, 2020 04:33Sayyid Abdul-Malik Badruddin al-Houthi, Kiongozi wa Ansarullah ya Yemen amesema, Mapinduzi ya Septemba 21 yalikuwa mwanzo wa kuondokana na zama zilizopita za giza na kupiga hatua mbele kuelekea kwenye ujenzi wa mustakabali unaoendana na misingi na thamani za watu wa Yemen.
-
Ansarullah ya Yemen: Kuanzisha uhusiano na utawala haramu wa Israel ni usaliti kwa Palestina
Sep 17, 2020 22:13Msemaji wa Harakati ya Ansarullah ya Yemen amesema kuwa, kuanzisha uhusiano wa kawaida na utawala haramu wa Israel ni khiyana na usaliti wa wazi kwa taifa la Palestina.
-
Ansarullah ya Yemen: Saudia na Imarati zina nafasi haribifu katika eneo la Asia Magharibi
Sep 14, 2020 22:05Katibu Mkuu wa harakati ya Ansarullah ya Yemen ametahadharisha kuhusu hatari ya Saudi Arabia na Imarati na nafasi haribifu ya nchi hizo katika eneo la magharibi mwa Asia.
-
Ansarullah yataka kuundwa muungano wa Kiislamu wa kupinga uhusiano na Israel
Sep 12, 2020 02:26Msemaji wa harakati ya wananchi wa Yemen ya Ansarullah ametoa wito wa kuundwa muungano wa Kiislamu dhidi ya hatua yoyote ya kuanzishwa uhusiano baina ya nchi za Kiarabu na utawala haramu wa Israel.
-
Umuhimu wa mashambulizi ya Ansarullah dhidi ya mji wa Abha huko Saudi Arabia
Sep 11, 2020 20:10Katika siku za karibuni jeshi na wapiganaji wa harakati ya Ansarullah nchini Yemen wamekuwa wakishambulia uwanja wa ndege wa Abha katika mkoa wa Asir huko kusini mwa Saudi Arabia kwa kutumia ndege zisizo na rubani (drone).
-
Ansarullah ya Yemen yapiga kwa kombora, droni maeneo ya kistratajia Riyadh, Saudia
Sep 11, 2020 00:15Harakati ya Ansarullah ya Yemen imelenga kwa kombora la balestiki na ndege zisizo na rubani (droni) maeneo ya kistratajia ndani ya mji mkuu wa Saudi Arabia, Riyadh.
-
Al Houthi: Saudi Arabia na Imarati ni vinara wa unafiki
Aug 30, 2020 22:43Katibu Mkuu wa harakati ya wananchi wa Yemen ya Ansarullah amesema kuwa Saudi Arabia na Imarati ni vinara wa kambi ya unafiki.
-
Ansarullah: Kimya cha Jumuiya ya Nchi za Kiarabu mbele ya mapatano ya Abu Dhabi-Tel Aviv kinaaibisha
Aug 17, 2020 02:16Msemaji wa harakati ya Ansarullah ya wananchi wa Yemen amesema kuwa kimya cha Jumuiya ya Nchi za Kiarabu (Arab League) mbele ya hatua ya Umoja wa Falme za Kiarabu (Imarati) ya kuanzisha uhusiano na utawala haramu wa Israel ni fedheha na aibu kubwa.