-
Upinzani wa China kwa hatua ya Marekani ya kuishambulia kijeshi Yemen
Jan 26, 2024 23:04Wang Wenbing, Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China amesema, Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa halijatoa kibali kwa mtu yeyote kutumia nguvu dhidi ya Yemen, akimaanisha hujuma na mashambulio ya kijeshi yanayofanywa na Marekani na Uingereza dhidi ya ngome na vituo vya harakati ya Ansarullah ya Yemen.
-
Ansarullah yaitaka UN iwaondoe Yemen wafanyakazi wake raia wa US, UK
Jan 25, 2024 07:42Harakati ya Ansarullah imeziagiza Marekani na Uingereza ziwaondoea nchini Yemen raia wake wanaoufanyia kazi Umoja wa Mataifa katika mji mkuu wa nchi hiyo ya Kiarabu, Sana'a.
-
Iran yaikosoa US kwa kuiweka Ansarullah katika orodha ya 'ugaidi'
Jan 19, 2024 00:00Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amelaani vikali hatua ya Marekani ya kuiweka Harakati ya Ansarullah ya Yemen kwenye orodha ya kile inachokiita "makundi ya kigaidi" na kueleza kwamba, kitendo hicho ni katika mfululizo wa hatua za Washington za kuuunga mkono utawala wa kigaidi wa Israel.
-
Ansarullah ya Yemen: Ni fakhari kwetu kuitwa magaidi na utawala wa kigaidi wa Marekani kwa sababu ya Palestina
Jan 18, 2024 03:13Ofisi ya Harakati ya Ansarullah ya Yemen imetoa mjibizo kwa hatua ya Marekani ya kuiweka harakati hiyo kwenye orodha ya kile inachokiita "makundi ya kigaidi" na kueleza kwamba hatua hiyo ya Washington haina thamani wala itibari yoyote.
-
Ansarullah: Marekani haijafikia malengo yake kwa kuishambulia Yemen
Jan 13, 2024 08:22Mkuu wa shirika la habari la Harakati ya Ansarullah ya Yemen amesema mashambulizi ya Marekani dhidi ya vituo vya makombora ya harakati hiyo ya muqawama hayajafanikiwa, na kwamba Washington imeshindwa kufikia malengo yake kwa hujuma hizo.
-
Ansarullah: Marekani na Uingereza zijiandae 'kulipa gharama kubwa' kwa kuishambulia Yemen
Jan 12, 2024 04:14Harakati ya Muqawama ya Ansarullah ya Yemen imezilaani vikali Marekani na Uingereza baada ya kufanya mashambulizi makali dhidi ya vituo vyake ndani ya Yemen, na kuonya kuwa vituo vya kijeshi vya nchi hizo vilivyoko katika eneo vitashambuliwa iwapo zitafanya uchokozi zaidi.
-
US, UK zashambulia vituo vya Ansarullah Yemen kwa sababu ya msimamo wake wa kuwahami Wapalestina
Jan 12, 2024 00:25Marekani na Uingereza zimeshambulia vituo kadhaa vya harakati ya Ansarullah kukabiliana na hatua ya harakati hiyo ya wananchi wa Yemen ya kuzishambulia meli zenye uhusiano na utawala haramu wa Kizayuni wa Israel, kwa sababu ya vita vya mauaji ya kimbari na ya halaiki unavyoendesha utawala huo dhalimu dhidi ya Wapalestina wa Gaza.
-
Ansarullah ya Yemen: Maji ya Kimataifa ni salama kwa meli zote isipokuwa za utawala wa Kizayuni wa Israel
Dec 29, 2023 06:59Harakati ya Muqawama wa Kiiislamu ya Ansarullah ya Yemen imesisitiza kuwa njia za majini za kimataifa ni salama kwa meli zote, isipokuwa meli za utawala haramu wa Kizayuni wa Israel au zile zinazoelekea katika ardhi zinazokaliwa kwa mabavu na utawala huo.
-
Ansarullah: Msimu wa baridi kali umekaribia Ulaya; tukichokozwa tutapiga visima na meli za mafuta na gesi
Dec 20, 2023 07:44Mmoja wa viongozi waandamizi wa Harakati ya Ansarullah ya Yemen amezionya nchi mbili za Kiarabu kwamba zisithubutu kuingia kwenye muungano wa Bahari Nyekundu wa Marekani na imetangaza wazi kwamba, kama Yemen itashambuliwa, basi harakati hiyo itajibu kwa kupinga visima na meli za maafuta na gesi na haitojali kwamba msimu wa baridi kali umekaribia barani Ulaya.
-
Jeshi la Yemen: Tutalenga na kuteka meli zote za Israel katika Bahari Nyekundu
Nov 19, 2023 23:58Msemaji wa Jeshi la Yemen amesema vikosi vya nchi hiyo vitashambulia na kuteka meli zote zinazomilikiwa au kusimamiwa na kampuni za utawala wa Kizayuni wa Israel, ikiwa ni hatua kuliunga mkono taifa la Palestina, wakati huu ambapo Wazayuni wanaendelea kumwaga damu za Wapalestina katika Ukanda wa Gaza.