-
EU yazidi kuandamwa na lawama kwa msimamo wake wa upendeleo katika kadhia ya Gaza
Nov 22, 2023 00:01Mkuu wa Sera za Nje wa Umoja wa Ulaya ametahadharisha kuwa umoja huo unakabiliwa na chuki zinazoongezeka katika Ulimwengu wa Kiislamu na nje yake kutokana na shutuma za kuegemea upande wa utawala wa Kizayuni wa Israel na kuwa na misimamo ya undumilakuwili kuhusiana na Vita vya Gaza.
-
Ukosolewaji mkali wa undumakuwili wa Magharibi kuhusu kadhia ya Israel na Wapalestina
Nov 21, 2023 03:42Waziri Mkuu wa Ireland, Leo Varadkar amekosoa vikali undumilakuwili wa nchi za Magharibi na kusema kuwa Umoja wa Ulaya na madola ya Magharibi yanashughulikia masuala yanayohusiana na Israel na Palestina kwa undumilakuwili wa wazi.
-
Mbunge wa Kizayuni: Kuuliwa watoto Gaza ni jinai
Nov 19, 2023 03:16Mbunge wa utawala wa Kizayuni ameyataja mauaji ya watoto na wanawake wasio na hatia katika Ukanda wa Ghaza yanayofanywa na jeshi la utawala huo kuwa ni jinai.
-
Azimio la Baraza la Usalama kuhusu vita vya Gaza: Makubaliano ya kiwango cha chini
Nov 16, 2023 23:47Uzembe wa Umoja wa Mataifa na hasa mkwamo katika Baraza la Usalama la umoja huo ambao una jukumu muhimu la kulinda amani na usalama wa kimataifa, kuhusu vita vya Gaza, jinai za kivita na mauaji ya kimbari ya Wapalestina yanayofanywa na utawala wa Kizayuni, umekosolewa vikali kimataifa.
-
SEPAH: Jinai za Wazayuni haziwezi kuzuia ushindi wa Wapalestina; Iran imejiandaa kwa hali zote
Nov 13, 2023 23:05Kamanda wa Kikosi cha Anga za Mbali cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu SEPAH amesema kuwa, kamwe jinai za utawala wa Kizayuni haziwezi kuzuia ushindi wa Wapalestina, na pia Marekani itambuwe kuwa, Jamhuri ya Kiislamu ina nguvu kubwa na hakuna mtu anayeweza kuliteteresha taifa la Iran kwa vitisho vyake.
-
Kuadhibiwa waungaji mkono wa Palestina katika vyuo vikuu vya Marekani
Nov 12, 2023 23:17Licha ya madai ya kuheshimiwa uhuru wa kujieleza katika nchi za Magharibi ikiwemo Marekani, lakini ukweli wa mambo ni kwamba kuna mistari miekundu katika uwanja huo, likiwemo suala la kutetea kadhia ya Palestina, ambapo waungaji mkono wa taifa hilo linalodhulumiwa hukabiliwa na vikwazo vya aina mbalimbali vikiwemo vya kuadhibiwa na kufungwa jela.
-
Maafisa zaidi ya 1,000 wa serikali ya Marekani wamwandikia barua Biden kumtaka akomeshe jinai za Wazayuni
Nov 12, 2023 03:24Wafanyakazi zaidi ya elfu moja wa Shirika la Maendeleo la Kimataifa la Marekani wamesaini barua ya wazi na kumpelekea rais wa nchi hiyo Joe Biden kumtaka asimamishe jinai na mashambulizi ya utawala wa Kizayuni katika Ukanda wa Gaza na kusitishwa vita haraka katika Ukanda huo.
-
Kuongezeka hasira za kimataifa kuhusu jinai za utawala wa Kizayuni huko Gaza
Nov 11, 2023 23:37Sambamba na kuendelea vitendo vya jinai vya utawala wa Kizayuni katika Ukanda wa Gaza, ambavyo hadi sasa vimepelekea kuuawa shahidi zaidi ya Wapalestina elfu 11 na kujeruhiwa wengine zaidi ya elfu 27, hasira na ukosoaji wa kimataifa unaendelea kuongezeka kwa kadiri kwamba mbali na maandamano makubwa yanayofanyika katika pambe tofauti za dunia, baadhi ya wanasiasa wa Magharib pia wanaukosoa utawala huo kutokana na ukatili wake wa kutisha dhidi ya Wapalestina wasio na hatia.
-
WHO: Katika kila dakika 10 jeshi la Israel linaua mtoto mmoja Gaza
Nov 11, 2023 23:25Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Afya Duniani (WHO) Tedros Adhanom Ghebreyesus amesema, mtoto mmoja wa Kipalestina huuawa kwa wastani wa kila dakika 10 katika Ukanda wa Gaza na akatoa indhari kwa kusema "hakuna mahali popote na hakuna mtu yeyote aliye salama" chini ya mashambulizi ya Israel kwenye eneo hilo lililozingirwa.
-
Rais Raisi: Vita vya Gaza ni makabiliano kati ya mhimili wa sharafu na mhimili wa uovu
Nov 11, 2023 11:28Rais Ebrahim Raisi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesisitiza katika kikao cha pamoja cha Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu OIC na Jumuiya ya Nchi za Kiarabu kwamba: kadhia ya Gaza ni makabiliano baina ya mhimili wa sharafu na mhimili wa uovu, na kila mtu anapaswa abainishe yuko upande gani.