-
Wanaharakati waandamana Chicago, Marekani kulaani hujuma za Israel, Gaza
Nov 22, 2019 23:08Makumi ya wanaharakati wamefanya maandamano katika mji wa Chicago jimboni Illinois nchini Marekani, kulaani mashambulizi ya anga yaliyofanywa hivi karibuni na ndege za jeshi katili la Israel dhidi ya Wapalestina wa Ukanda wa Gaza.
-
Hamas: Tutalipiza kisasi cha damu za mashahidi wote wa Ukanda wa Ghaza
Nov 18, 2019 23:11Mkuu wa Ofisi ya Kisiasa ya Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS amesema kuwa harakati hiyo itaendeleza mapambano dhidi ya utawala wa Kizayuni na italipigiza kisasi cha damu yote ya wananchi wa Palestina iliyomwagwa na Israel huko Ghaza.
-
Mashambulizi ya anga ya Israel yaua shahidi makumi ya Wapalestina Gaza
Nov 13, 2019 23:13Ndege za kivita za utawala wa Kizayuni wa Israel jana Jumanne na kwa siku ya pili mfufulizo zilitekeleza mashambulizi ya anga zaidi ya 50 katika Ukanda wa Gaza, na kuua shahidi makumi ya Wapalestina.
-
Wanamuqawama wa Palestina wajibu mapigo baada ya Israel kumuua shahidi kamanda wa Jihad Islami
Nov 12, 2019 04:37Wanamuqawama wa Palestina wametoa jibu kali baada ya jeshi katili la utawala wa Kizayuni wa Israel kumuua shahidi kamanda wa ngazi za juu wa Harakati ya Jihadul-Islam ya Palestina katika Ukanda wa Gaza.
-
Shambulizi la anga la Israel laua na kujeruhi Wapalestina Gaza
Nov 02, 2019 08:55Mashambulizi ya anga ya ndege za kivita za utawala wa Kizayuni wa Israel yamepelekea kuuawa shahidi raia mmoja wa Palestina na kujeruhiwa wengine wawili.
-
Askari wa Israel wamuua shahidi Mpalestina katika 'Maandamano ya Haki ya Kurejea'
Oct 05, 2019 03:22Wanajeshi wa utawala wa Kizayuni wa Israel wamempiga risasi na kumuua shahidi Mpalestina ambaye alikuwa anashiriki katika Ijumaa ya 77 ya 'Maandamano Makubwa ya Haki ya Kurejea' katika Ukanda wa Ghaza. Wapalestina wengine 40 wamejeruhiwa wakati wanajeshi hao wa utawala wa Kizayuni waliposhambulia maandamano hayo ya amani.
-
Hamas: Lengo la Israel la kuishambulia Ghaza ni kupotosha fikra za waliowengi
Aug 17, 2019 03:32Msemaji wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (Hamas) amesema kuwa, lengo la utawala wa Kizayuni la kutekeleza mashambulizi dhidi ya Ghaza ni kutaka kupotosha fikra za waliowengi kuhusu oparesheni za muqawama zilizofanywa hivi karibuni katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan.
-
Wanajeshi wa utawala wa Kizayuni wahofia kufanya kazi katika mipaka ya Ghaza
Aug 02, 2019 20:55Redio ya jeshi la utawala wa Kizayuni imesisitiza kuwa wanajeshi wa utawala huo hawana hamu ya kuhudumu katika mipaka ya Ukanda wa Ghaza na wanafadhilisha kufanya kazi katika maeneo mengine.
-
B'Tselem: Jeshi la Israel huwaua kwa makusudi Wapalestina wanaoandamana Ghaza
Jul 28, 2019 03:04Kituo cha Haki za Binadamu katika ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu (Israel) kimeripoti kuwa jeshi la utawala wa Kizayuni huwaua kwa makusudi na bila ya sababu raia wa Palestina wanaondamana katika maandamano yao ya amani ya haki ya kurejea katika mipaka ya Ghaza.
-
Kubomolewa nyumba za Wapalestina baada ya vita; jinai zisizo na kikomo za Israel
Jul 23, 2019 23:26Utawala wa Kizayuni wa Israel baada ya kushindwa katika vita vilivyodumu kwa muda wa siku mbili tu, hivi sasa umeanzisha duru mpya ya jinai zake dhidi ya Wapalestina kwa kubomoa nyumba za wananchi hao madhulumu.