Mohammad Shtayyeh: Israel inataka kuwasahaulisha walimwengu umuhimu wa Quds
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i53455-mohammad_shtayyeh_israel_inataka_kuwasahaulisha_walimwengu_umuhimu_wa_quds
Waziri Mkuu wa Mamlaka ya Ndani ya Palestina amesema kuwa, lengo la utawala wa Kizayuni la kuushambulia Ukanda wa Ghaza ni kutaka kuwasahaulisha walimwengu jinai zake na umuhimu wa mji mtakatifu wa Quds.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
May 13, 2019 09:57 UTC
  • Mohammad Shtayyeh: Israel inataka kuwasahaulisha walimwengu umuhimu wa Quds

Waziri Mkuu wa Mamlaka ya Ndani ya Palestina amesema kuwa, lengo la utawala wa Kizayuni la kuushambulia Ukanda wa Ghaza ni kutaka kuwasahaulisha walimwengu jinai zake na umuhimu wa mji mtakatifu wa Quds.

Shirika la habari la Fars limemnukuu Mohammad Shtayyeh akisema hayo na huku akipongeza misaada ya kibinadamu wanayotumiwa wananchi wa Ghaza ameongeza kuwa: Israel inaushambulia mara kwa mara Ukanda wa Ghaza ili kuwashaulisha walimwengu jinai zake kama za kuwapora Wapalestina ardhi zao na kujenga vitongoji vya walowezi wa Kizayuni na kujaribu kuangamiza muundo wa Kiarabu na Kiislamu wa Msikiti wa al Aqsa na wa mji wa Baytul Muqaddas ili kwa njia hiyo iweze kuendelea njama zake bila ya wasiwasi.

Wanajeshi akatili wa Israel wanafanya jinai kubwa dhidi ya Wapalestina

Waziri Mkuu huyo wa Mamlaka ya Ndani ya Palestina amelitaka Shirika la Msalaba Mwekundu Duniani kutoa mchango mkubwa katika juhudi za kufichua jinai za Israel kwa Wapalestina na uvunjaji wake mkubwa wa haki za binadamu.

Wapalestina 31 wakiwemo wanawake na watoto wadogo kadhaa waliuawa shahidi na wengine 77 kujeruhiwa katika mashambulizi ya hivi karibuni ya Israel katika Ukanda wa Ghaza.

Makundi ya Palestina nayo yalitoa majibu makali kwa utawala wa Kizayuni kwa kuvitwanga vitongoji vya walowezi wa Kizayuni kwa makombora na maroketi zaidi ya 600 na kupelekea kwa uchache walowezi 105 wa Kizayuni kuuawa na kujeruhiwa.