-
Sayyid Hassan Nasrullah: Kukabiliana na Marekani ni lazima kuwe kwa pande zote na kuhusishe sekta zote
Feb 16, 2020 12:36Katibu Mkuu wa Harakati ya Kiislamu ya Hizbullah ya Lebanon amesema kuwa Marekani ni muhusika wa vita vyote eneo la Asia Magharibi na amesisitiza kuwa, ni lazima kuendesha muqawama katika pande zote kukabiliana na utawala huo wa kibeberu wa Marekani.
-
"ISIS walitaka kushambulia ubalozi wa Marekani Lebanon na kuisingizia Hizbullah"
Jan 24, 2020 02:45Gazeti la al Jamhuriyyah la Lebanon limefichua kuwa, genge la kigaidi na ukufurishaji la Daesh (ISIS) lilikuwa limepanga njama za kushambulia ubalozi wa Marekani mjini Beirut ili kuibebesha lawama harakati ya Kiislamu ya nchi hiyo Hizbullah hasa baada ya Marekani kumuua kigaidi Luteni Jenerali Qassem Soleimani, Kamanda wa Kikosi cha Quds, cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu SEPAH.
-
Hizbullah: Maelfu ya Maqassim Soleimani watalipiza kisasi cha damu yake
Jan 16, 2020 04:28Naibu Katibu Mkuu wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Hizbullah ya Lebanon ametangaza kuwa, adui asijidanganye kwamba, kwa kumuua Luteni Jenerali Qassim Soleimani njia ya mwanamapambano huyo haitaendelea, bali maelfu ya watu mfano wake watajitokeza kulipiza kisasi cha damu yake.
-
Waziri wa Mambo ya Nje wa Lebanon aunga mkono misimamo ya Hizbullah
Dec 17, 2019 09:12Waziri wa Mambo ya Nje wa Lebanon Gebran Bassil ameunga mkono misimamo ya harakati ya muqawama ya Hizbullah katika uga wa kisiasa na kijeshi wa nchi hiyo.
-
Hizbullah yapinga masharti ya Marekani kwa ajili ya kuundwa serikali mpya ya Lebanon
Nov 26, 2019 04:32Harakati ya Hizbullah ya Lebanon imepinga masharti yaliyotolewa na Marekani kwa ajili ya kuundwa serikali mpya ya Lebanon.
-
Sayyid Hassan Nasrullah: Maadui wamejawa hofu kwa kushuhudia matembezi ya Arubaini
Oct 19, 2019 10:06Katibu Mkuu wa Harakati ya Hizbullah ya Lebanon Sayyid Hassan Nasrullah amesisitiza kuwa, uwepo wa mamilioni ya watu mjini Karbala ni jambo lisilo na mfano katika historia na kwamba Marekani, utawala haramu wa Kizayuni, mabeberu na madhalimu wa dunia wanahisi hofu kubwa kwa kushuhudia matembezi ya mamilioni ya watu katika Arubaini ya Imam Hussein (as).
-
Hizbullah: Hatutosalimu amri mbele ya mashinikizo ya Marekani
Oct 10, 2019 08:37Naibu Mkuu wa Baraza la Utendaji la Harakati ya Hizbullah ya Lebanon amesisitiza kuwa vikwazo vya Marekani haviwezi kudhoofisha imani na ahadi yake ya kulinda nchi na raia.
-
Aoun atetea oparesheni ya Hizbullah dhidi ya utawala wa Kizayuni
Oct 02, 2019 04:35Rais wa Lebanon amekutana na Mjumbe wa Umoja wa Mataifa katika masuala ya Lebanon na kutetea oparesheni iliyofanywa na harakati ya Hizbullah ya nchi hiyo dhidi ya chokochoko za utawala wa Kizayuni.
-
Sheikh Nabil Qaouk: Vikwazo vya Marekani havijawa na taathira yoyote kwa Hizbullah
Sep 28, 2019 22:59Mjumbe wa Baraza la Utendaji la Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Hizbullah ya Lebanon amesisitiza kuwa, vikwazo vya Marekani dhidi ya harakati hiyo havijawa na taathira na kwamba, vikwazo hivyo ni matokeo ya kukata tamaa Washington.
-
Lebanon yapongeza hatua ya harakati ya Hizbullah ya kulinda nchi dhidi ya Israel
Sep 21, 2019 07:38Waziri wa Mambo ya Nje wa Lebanona sambamba na kubainisha kwamba siasa za serikali ya Beirut ni kujiepusha na aina yoyote ya vita katika eneo, amepongeza hatua ya harakati ya Kiislamu ya Hizbullah ya kulinda nchi hiyo mkabala na shambulio la hivi karibuni la ndege zisizo na rubani za utawala haramu wa Kizayuni.