Jeshi la utawala wa Kizayuni lafuta mazoezi ya kijeshi likihofia kushambuliwa na Hizbullah
(last modified Thu, 23 Jul 2020 08:04:24 GMT )
Jul 23, 2020 08:04 UTC
  • Jeshi la utawala wa Kizayuni lafuta mazoezi ya kijeshi likihofia kushambuliwa na Hizbullah

Duru za habari za utawala wa Kizayuni zimetangaza kuwa wanajeshi wa Israel wamefuta mazoezi waliyopanga kufanya wakihofia kushambuliwa na harakati ya Hizbullah ya Lebanon.

Harakati ya Muqawama ya Hizbullah ya Lebanon imetoa taarifa na kueleza kuwa mwanapambano wao mmoja ameuliwa shahidi katika shambulio la anga la utawala wa Kizayuni karibu na uwanja wa ndege wa Damascus mji mkuu wa Syria. 

Mauaji ya mwanamapambano wa Hizbullah yaliyofanywa na Israel karibu na uwanja wa ndege wa Damascus, Syria 

Vyombo vya habari vya utawala wa Kizayuni vimetangaza kuwa, makamanda wa jeshi la Israel wamefuta mazoezi ya kijeshi yaliyokuwa yamepangwa kufanyika katika mipaka ya kaskazini mwa Palestina inayokaliwa kwa mabavu na Lebanon.  

Televisheni ya Russia al Yaum pia imekinukuu chombo kimoja cha karibu na Hizbullah na kuripoti kuwa, harakati hiyo ya muqawama ya Lebanon imejiweka tayari kujibu mauaji ya mpiganaji wao huko Syria. Habari nyingine zinasema kuwa, wanajeshi kadhaa wa Israel wameangamia na kujeruhiwa katika tukio la baada ya gari yao aina ya Jeep kupinduka. Jeshi la utawala wa Kizayuni limekataa kutoa maelezo zaidi kuhusu kuangamia wanajeshi hao na kutosheka tu kwa kusema kuwa uchunguzi wa polisi unaendelea katika uwanja huo. 

Tags