Makumi ya Wapalestina wauawa shahidi katika shambulio la kikatili la utawala wa Kizayuni kwenye kambi ya Jabalia
(last modified Tue, 22 Oct 2024 08:06:22 GMT )
Oct 22, 2024 08:06 UTC
  • Makumi ya Wapalestina wauawa shahidi  katika shambulio la kikatili la utawala wa Kizayuni kwenye kambi ya Jabalia

Jeshi la Kizayuni limeshambulia kwa makombora raia wanaoishi katika kambi ya Jabalia na kulenga nyumba moja kaskazini mwa Gaza na kuwaua Wapalestina 26, baadhi yao wakiwa ni watoto.

Mashambulizi ya makombora ya utawala huo katika shule ya Jabalia wanakoishi wakimbizi wa Kipalestina yamesababisha kuuawa shahidi Wapalestina 7 na kujeruhi wengine wengi.

Wapalestina 6, ambao baadhi yao walikuwa watoto, wameuawa shahidi na wengine kadhaa kujeruhiwa katika shambulio hilo la kinyama  lilitekelezwa na utawala dhalimu wa  Israel dhidi ya mkusanyiko wa raia waliokuwa wakijaribu kuchota maji ya kunywa katika mji wa Jabalia.

Katika kambi ya Jabalia, Wapalestina 4 wameuawa shahidi katika hujuma ya anga ya Wazayuni katika viunga vya Hospitali ya Alyemen Assaeed.

Katika mji wa Ukanda wa  Gaza, Wapalestina 9 wameuawa shahidi na makumi ya  wengine  wamejeruhiwa kutokana na kushambuliwa nyumba moja kaskazini mwa mji huo.

Wakati huo huo, vyanzo vya Wapalestina viliripoti  jana Jumanne asubuhi kwamba vikosi vya Israeli viliwakamata Wapalestina 13 katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan kwa kuvamia kambi ya al-Arub kaskazini mwa mji wa al-Khalil.

Kadhalika, jeshi la utawala wa Kizayuni limeshambulia kambi ya Nablus na Balata mashariki mwa Nablus, kambi ya Al Arab iliyoko kaskazini mwa al-Khalil, na mji wa Kobar kaskazini mwa Ramallah.

Tags