Hizbullah ya Lebanon yafanya shambulio kali katika kambi ya kijasusi ya kijeshi huko Tel Aviv
(last modified Tue, 22 Oct 2024 07:57:08 GMT )
Oct 22, 2024 07:57 UTC
  • Hizbullah ya Lebanon yafanya shambulio kali  katika  kambi ya kijasusi ya kijeshi huko Tel Aviv

Harakati ya Muqawama ya Hizbullah ya Lebanon imefanya shambulizi kali la makombora dhidi ya kambi ya kijasusi ya kijeshi ya utawala dhalimu wa Israel katika viunga vya mji wa Tel Aviv katika ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu na Israel.

Harakati hiyo ilitangaza jana Jumatatu kuwa imetekeleza shambulio hilo kali la kulipiza kisasi katika Kambi ya Glilot ya utawala wa Kizayuni ambayo ni kitengo cha ujasusi cha kijeshi  nambari  8200 cha Israel.
Imesema imefanya oparesheni hiyo "kwa ajili ya kuunga mkono watu wetu shupavu wa Palestina katika Ukanda wa Gaza na kuwalinda watu wa Lebanon."

Shambulio hilo limekuja katika mululizo wa "oparesheni za Khaybar za kujibu uchokozi na mauaji ya kinyama  yanayofanywa na adui wa Kizayuni dhidi ya watu wa Ukanda wa Gaza na Lebanon."

Utawala habithi  wa Israel umezidisha mashambulizi yake dhidi ya Lebanon tangu mwezi Oktoba mwaka jana, jambo lililosababisha Hizbullah kuanza kujibu kwa kuvurumisha mamia ya makombora dhidi ya maeneo nyeti yaliyoko katika ardhi zinazokaliwa kwa mabavu na kuwalenga wanajeshi wa Israel wanaojaribu kusonga mbele katika maeneo ya kusini mwa Lebanon.