Rais Paul Biya arejea Cameroon, baada ya kutoweka kwa takribani wiki 6 na kusababisha wasiwasi wa kiafya
(last modified Tue, 22 Oct 2024 07:41:17 GMT )
Oct 22, 2024 07:41 UTC
  • Rais Paul Biya arejea Cameroon, baada ya kutoweka kwa takribani  wiki 6 na kusababisha wasiwasi wa kiafya

Baada ya kukosekana kwa muda wa wiki 6 na kusababisha wasiwasi juu ya afya yake na mahali alipo, Rais Paul Biya wa Cameroon hatrimaye amerejea nchini.

Rais huyo mwenye umri wa miaka 91 amewasili mnchini kutokea Geneva, Uswisi  akiwa ameandamana  na mkewe Chantal Biya, na wala hakuzungumza na wananchi. Pamoja na hayo aliwapungia mkono wafuasi wake  waliokusanyika karibu na gari lake lilipokuwa likiondoka kwenye uwanja wa ndege katika mji mkuu wa Cameroon  Yaounde.

Maelfu ya wafuasi wa chama tawala cha Cameroon (People's Democratic Movement) walikuwa wamekusanyika barabarani kote kutoka uwanja wa ndege hadi ikulu ya rais huyo.

Baadhi ya watu kwenye umati huo, walikuwa wamebeba mabango ya kumkaribisha Rais, na kutoa salamu zao za heri.

Kutoweka rais huyo  kutoka Cameroon kulizua uvumi ulioenea kwamba alikuwa mgonjwa mahututi

Lakini maafisa wa nchi hiyo walitoa taarifa wakisisitiza kuwa alikuwa mzima wa afya, na kusisitiza kuwa usalama wake lilikuwa suala la usalama wa taifa.