Iran yaliandikia barua Baraza la Usalama ikilaani chokochoko za US
(last modified Tue, 22 Oct 2024 07:16:30 GMT )
Oct 22, 2024 07:16 UTC
  • Iran yaliandikia barua Baraza la Usalama ikilaani chokochoko za US

Balozi na Mwakilishi wa Kudumu wa Iran katika Umoja wa Mataifa amekosoa vikali matamshi ya hivi karibuni ya Rais Joe Biden wa Marekani kuhusiana na njama ovu ya utawala haramu wa Israel dhidi ya Tehran na kusisitiza kuwa, matamshi hayo "yanatia wasiwasi sana na ni ya kichochezi."

Amir Saeid Iravani amesema katika barua yake hiyo kwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa na Baraza la Usalama la umoja huo kuwa, Marekani inabeba dhima kamili ya kushadidi taharuki katika eneo na kwa kuupa silaha utawala wa Israel ili utekeleza vitendo vya kichokozi dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu.

Mwanadiplomasia huyo wa ngazi ya juu wa Iran ameyataja matamshi hayo ya Biden kuwa "ya kutisha na ya kichochezi" akisisitiza kuwa, yanaonyesha "ridhaa ya kimya kimya ya Marekani na uungaji mkono wa wazi kwa uchokozi wa kijeshi wa Israel dhidi ya Iran."

Hivi karibuni, Rais wa Marekani, Joe Biden alidai kwamba alikuwa na wazo bora la jinsi na lini Israel itaishambulia Iran. Iravani ameongeza kuwa, "Taarifa kama hizo zinapingana na madai ya mara kwa mara ya Marekani kwamba inataka kupunguzwa hali ya taharuki katika eneo hili."

Rais wa Marekani, Joe Biden

Hivi karibuni pia, Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran alisema Marekani inapasa kubebeshwa dhima ya shambulio lolote tarajiwa la Israel dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu.

Sayyid Abbas Araghchi akirejelea matamshi hayo ya Biden alieleza bayana kwamba, upande au mtu yeyote mwenye ufahamu wa jinsi na lini Israel itaishambulia Iran, anapaswa kuwajibishwa na kubeba dhima ya taathira za shambulio hilo.

 

Tags