Vyama vya Siasa Tunisia vyalaani hatua ya Ujerumani dhidi ya Hizbullah
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i60806-vyama_vya_siasa_tunisia_vyalaani_hatua_ya_ujerumani_dhidi_ya_hizbullah
Vyama vitano vya kisiasa nchini Tunisia vimelaani vikali hatua ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Ujerumani ya kuiorodhesha Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Hizbullah ya Lebanon kama kundi la kigaidi.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
May 06, 2020 03:25 UTC
  • Vyama vya Siasa Tunisia vyalaani hatua ya Ujerumani dhidi ya Hizbullah

Vyama vitano vya kisiasa nchini Tunisia vimelaani vikali hatua ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Ujerumani ya kuiorodhesha Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Hizbullah ya Lebanon kama kundi la kigaidi.

Shirika la habari la IRNA limenukuu taarifa ya vyama hivyo inayosema kuwa: Ujerumani imechukua hatua hiyo ili kufuata amri ya utawala wa Kizayuni wa Israel, na kuifuata kibubusa Marekani.

Taarifa hiyo imeutaja uamuzi huo wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Ujerumani dhidi ya Hizbullah ya Lebanon kama 'Uzayuni wa kimataifa'.

Vyama hivyo vya kisiasa vya Tunisia vimesema tangazo hilo la Ujerumani limetolewa kutokana na nafasi muhimu ya harakati hiyo ya muqawama ya kukabiliana na uvamizi wa Wazayuni.

Aidha vimelitaka taifa la Tunisia, ulimwengu wa Kiarabu na nchi zote huru duniani kusimama dhidi ya hatua za aina hiyo za madola ya kibeberu.

Uungaji mkono wa wananchi wa Lebanon kwa Hizbullah

Tangazo hilo la Wizara ya Mambo ya Ndani ya Ujerumani limekabiliwa na radiamali ya pamoja na mhimili wa muqawama katika eneo hili la Asia Magharibi, huku nchi mbali mbali duniani kama vile Iran, Yemen na Syria zikilaani hatua hiyo.

Uamuzi huo wa Ujerumani umechukuliwa sambamba na hatua ya utawala ghasibu wa Israel ya kuunganisha sehemu ya ardhi ya Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan na ardhi unazozikalia kwa mabavu huko Palestina.