-
Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Iran na Saudia wajadili mazungumzo ya Oman
Apr 15, 2025 08:06Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Iran na Saudi Arabia wamefanya mazungumzo ya simu na kujadiliana kuhusu uhusiano wa pande mbili na maendeleo ya kikanda na kimataifa.
-
Wanachuo wa Iran waendeleza maandamano ya kuiunga mkono Palestina
Apr 15, 2025 07:23Wanafunzi, maprofesa, wahadhiri na wafanyakazi wa Vyuo Vikuu vya mikoa ya Ardabil na Khorasan Kusini wamefanya maandamano ya kulaani ghasia na jinai zinazoendelea kufanywa na utawala wa Kizayuni wa Israel huko Gaza.
-
Iran: Ufaransa itoe maelezo ya kukamatwa Muirani, mtetezi wa Palestina
Apr 15, 2025 03:15Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amekosoa vikali kitendo cha Ufaransa cha kukataa kutoa maelezo ya kukamatwa Mahdieh Esfandiari, raia wa Iran anayeishi katika mji wa Lyon, kaskazini mwa magharibi mwa Ufaransa, zaidi ya mwezi mmoja baada kutiwa kwake mbaroni na vyombo vya usalama vya nchi hiyo ya Ulaya.
-
Zakharova:Tunasubiri kwa hamu safari ya ujumbe wa Iran mjini Moscow
Apr 14, 2025 13:10Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Russia amesema kuwa nchi hiyo inasubiri kwa hamu ziara ya ujumbe wa Iran mjini Moscow ili kukutana na kuzungumza na wenzao wa Russia.
-
Iran: Mazungumzo ya Oman ni chanya na ya matumaini; kuendelea wiki ijayo
Apr 13, 2025 02:40Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, Abbas Araqchi ameitaja duru ya kwanza ya mazungumzo yasiyo ya moja kwa moja kati ya Jamhuri ya Kiislamu na Marekani kuwa "chanya na yenye kuleta matumaini."
-
Wizara: Iran imezalisha mifumo ya ulinzi zaidi ya 900
Apr 13, 2025 02:21Wizara ya Ulinzi ya Iran imesema sekta ya ulinzi ya Jamhuri ya Kiislamu imeunda zaidi ya mifumo 900 ya ulinzi na zana za kijeshi; hatua inayoashiria ustawi wa kiwango kikubwa ikilinganishwa na kipindi cha kabla ya Mapinduzi ya Kiislamu ya 1979.
-
Iran: Tunataka makubaliano ya haki, heshima na usawa; Israel yaingiwa na kiwewe
Apr 12, 2025 12:20Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, Abbas Araghchi amesema Jamhuri ya Kiislamu inataka makubaliano ya haki na ya heshima, na yaliyojadiliwa kwenye mazingira ya usawa. Sayyid Araghchi amesema hayo kabla ya kuanza mazungumzo yasiyo ya moja kwa moja na wawakilishi wa Marekani.
-
Iraq: Tuna hamu ya kushirikiana na Iran kuimarisha utulivu wa kieneo
Apr 12, 2025 02:20Rais wa Iraq, Abdul Latif Rashid ametangaza utayarifu wa nchi yake wa kufanya kazi na kushirikiana na Iran ili kuhakikisha kuwa eneo hili la Asia Magharibi linakuwa na utulivu na usalama.
-
Kamanda wa Jeshi la Wanamaji: Uwezo wa kijeshi wa Iran uko juu sana
Apr 11, 2025 02:07Kamanda Mkuu wa Jeshi la Wanamaji la Iran, Admeli Shahram Irani amesema uwezo na nguvu za Jeshi la Iran zimefikia viwango vya juu ambavyo havijawahi kushuhudiwa.
-
Araqchi: Uhusiano wa Iran na Algeria uko imara, ni wa kihistoria
Apr 10, 2025 12:15Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema: Algeria ni nchi kubwa na yenye taathira katika Ulimwengu wa Kiislamu na kwamba uhusiano kati ya nchi hiyo na Iran ni mkubwa, imara na wa siku nyingi.