-
Rouhani: Kama si jitihada za IRGC, nchi mbili za eneo zingekuwa zinadhibitiwa na magaidi wa Daesh
Apr 10, 2019 03:34Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, iwapo Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) halingeingilia kati, basi kwa uchache mataifa mawili katika eneo hili la Asia Magharibi yangekuwa chini ya udhibiti wa kundi la kigaidi na kitakfiri la Daesh (ISIS).
-
Jamii ya kimataifa yaendelea kukosoa tangazo la Trump dhidi ya IRGC ya Iran
Apr 10, 2019 03:27Nchi mbalimbali duniani zimeendelea kukosoa hatua ya Rais Donald Trump ya kuliweka Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu IRGC katika orodha ya Marekani ya makundi ya kigaidi.
-
Sisitizo la Rais Putin la kuweko juhudi za pamoja za kuupatia ufumbuzi mgogoro wa Syria
Apr 10, 2019 02:09Mgogoro wa Syria na vita vya ndani vya kutwishwa nchi hiyo vilivyoanza 2011, ulipelekea Syria kugeuka na kuwa medani ya makabiliano baina ya Wamagharibi na waitifaki wao wa Kiarabu pamoja na Uturuki hapo awali dhidi ya mhimili wa muqawama ukijumuisha na Russia.
-
Larijani: Nchi za Kiislamu zimeitelekeza Palestina
Apr 08, 2019 03:28Spika wa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu (Bunge la Iran) Ali Larijani ameeleza kusikitishwa kwake na hatua ya nchi za Kiislamu ya kuitelekeza na kuiweka pembeni kadhia muhimu katika ulimwengu wa Kiislamu hivi sasa, ambayo ni Palestina.
-
Waziri Mkuu wa Iraq awasili Iran katika safari ya kuimarisha uhusiano wa Baghdad na Tehran
Apr 06, 2019 03:26Waziri Mkuu wa Iraq amewasili hapa nchini mapema leo katika ziara yenye lengo la kuimarisha uhusiano wa pande mbili wa Tehran na Baghdad.
-
Iran na Russia zaazimia kukabiliana na ubeberu wa vyombo vya habari wa Magharibi
Apr 05, 2019 23:26Mkuu wa Kitengo cha Kimataifa cha Shirika la Utangazaji la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran IRIB, amesema, kustawishwa ushirikiano wa vyombo vya habari kati ya Iran na Russia ni hatua yenye taathira kubwa katika kuhitimisha ukiritimba na ubeberu wa vyombo vya habari wa Magharibi.
-
Abu Turabi Fard: Mapinduzi ya Kiislamu yana nguvu na mahudhurio mpaka katika mipaka ya utawala wa Kizayuni
Apr 05, 2019 09:45Khatibu wa Sala ya Ijumaa iliyoswaliwa leo hapa mjini Tehran amesema kuwa, Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran yamebakia na kudumu katika misingi yake na kila siku yamekuwa yakipata ushindi mpya mbele ya madola yote ya kibeberu na hii leo mapinduzi haya yana mahudhurio yenye nguvu mpaka katika mipaka ya utawala wa Kizayuni wa Israel.
-
Madai ya Pompeo ya eti kuunga mkono hatua za IAEA kuhusiana na JCPOA
Apr 05, 2019 08:46Makubaliano ya nyuklia, yajulikanayo kama Mpango Kamili wa Pamoja wa Utekelezaji (JCPOA) yanahesabiwa kuwa ni makubaliano muhimu sana kwa ajili ya kudumisha amani na usalama wa kimataifa; lakini Marekani imekuwa ikiyachimba kwa dhamira ya kuyasambaratisha, hasa kutokana na hatua iliyochukuliwa na nchi hiyo tarehe 8 Mei, 2018 ya kutangaza kujitoa kwenye makubaliano hayo ya kimataifa.
-
Ndege ya misaada ya kibinadamu ya Ujerumani yawasili nchini Iran
Apr 05, 2019 02:51Balozi wa Ujerumaini nchini Iran ametangaza habari ya kuwasili ndege ya nchi hiyo yenye misaada ya kibinadamu kwa ajili ya wahanga wa mafuriko nchini Iran.
-
Zarif: Pompeo maliza kwanza matatizo ya ndani ya Marekani kabla ya kuingilia mambo ya wengine
Apr 04, 2019 23:44Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, wananchi wa Iran watatumia vizuri mshikamano na umoja wao katika kukabiliana vizuri na matatizo yaliyosababishwa na mafuriko ya hivi karibuni humu nchini.