Ndege ya misaada ya kibinadamu ya Ujerumani yawasili nchini Iran
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i52646-ndege_ya_misaada_ya_kibinadamu_ya_ujerumani_yawasili_nchini_iran
Balozi wa Ujerumaini nchini Iran ametangaza habari ya kuwasili ndege ya nchi hiyo yenye misaada ya kibinadamu kwa ajili ya wahanga wa mafuriko nchini Iran.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Apr 05, 2019 02:51 UTC
  • Ndege ya misaada ya kibinadamu ya Ujerumani yawasili nchini Iran

Balozi wa Ujerumaini nchini Iran ametangaza habari ya kuwasili ndege ya nchi hiyo yenye misaada ya kibinadamu kwa ajili ya wahanga wa mafuriko nchini Iran.

Shirika la habari la IRNA limetangaza habari hiyo na kuongeza kuwa, balozi wa Ujerumaini nchini Iran, Michael Klor Berchtold amesema katika ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Twitter kwamba, ndege yenye misaada ya kibinadamu ya Ujerumaini ambayo imetokea mjini Berlin ikiwa na misaada ya kibinadamu kwa ajili ya wahanga wa mafuriko nchini Iran, imewasili leo katika uwanja wa ndege wa Tehran.

Ameongeza kuwa Shirika la Msalaba Mwekundu la Ujerumaini limelipatia Shirika la Hilal Nyekundu la Iran boti 40 na vifaa vingine vya kiusalama.

Maafisa wa Hilal Nyekundu la Iran wakitoa misaada katika maeneo yaliyokumbwa na mafuriko humu nchini

 

Katika kipindi cha wiki mbili zilizopita, maeneo mbalimbali ya kaskazini, magharibi na kusini mwa Iran yamekukmbwa na mafuriko kutokana na mvua kubwa ambazo hazijawahi kutokea mfano wake humu nchini na kupelekea mito kufurika na kusababisha hasara za roho na mali za watu.

Licha ya kuweko maafa hayo ya kimaumbile, lakini Marekani imewazuia raia wa Iran wanaoishi nje ya nchi kuwafikishia wenzao misaada ya kibinadamu, na wakati huo huo viongozi hao wa Marekani wanadai kuwa eti hawana chuki na wananchi wa Iran.

Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, kitendo cha Marekani cha kuzuia misaada ya kibinadamu kwa wahanga wa mafuriko nchini Iran ni ugaidi wa kiuchumi.