-
Iran yazindua satalaiti 3 za Navak-1, Pars-1 iliyoboreshwa, na Pars-2
Feb 02, 2025 07:47Iran imezindua satalaiti tatu mpya wakati wa hafla iliyofanyika leo Jumapili kuadhimisha Siku ya Kitaifa ya Teknolojia ya Anga za Mbali.
-
Rais Pezeshkian atembelea mafanikio mapya ya anga na ulinzi ya Wizara ya Ulinzi
Feb 02, 2025 04:19Rais Masoud Pezeskhian mapema leo ametembelea maonyesho ya mafanikio ya Wizara ya Ulinzi. Ziara hii imefanyika leo Jumapili katika Shirika la Anga za Mbali la Iran katika kuadhimisha Siku ya Kitaifa ya Teknolojia ya Anga za Mbali.
-
IRGC yazindua kituo kipya cha chini ya ardhi cha makombora ya kruzi ya kuteketeza manowari za mashambulizi
Feb 02, 2025 00:07Kikosi cha Wanamaji cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) kimezindua kituo kipya cha chini ya ardhi katika maeneo ya mwambao wa kusini mwa Iran, kinachohifadhi makombora yaliyo tayari kuteketeza manowari za mashambulizi za adui katika eneo la kimkakati la majini.
-
Baraza la Mawaziri latangaza tena itiifu wao kwa malengo ya kiongozi mwasisi, Imam Khomeini
Feb 01, 2025 09:29Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na baraza lake la mawaziri mapema leo wamezuru haram ya mwasisi Jamhuri ya Kiislamu na kutangaza tena utiifu na mfungamano wao kwa thamani na malengo ya Imam Ruhullah Khomeini (Mwenyezi Mungu amrehemu).
-
Rais wa Iran: Sehemu kubwa ya matatizo ya Ulimwengu wa Kiislamu yanasababishwa na kuwa mbali na mafundisho ya Qur'ani
Jan 31, 2025 23:37Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema katika ujumbe wake katika hafla ya kumalizika duru ya 41 ya Mashindano ya Kimataifa ya Qur'an katika mji wa Mash'had hapa nchini kuwa: Sehemu kubwa ya matatizo ya Ulimwengu wa Kiislamu hii leo ni matokeo ya kuwa mbali na mafundisho ya Qur'ani.
-
Iran yaonya: Shambulio dhidi ya vituo vyetu vya nyuklia litasababisha 'vita vitakavyoenea katika eneo'
Jan 31, 2025 23:37Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran Sayyid Abbas Araghchi ametoa onyo kali kuhusu matokeo mabaya ya kitendo cha uchokozi kinachoweza kufanywa, ambacho kinaweza kuuhusisha utawala wa Kizayuni wa Israel na Marekani dhidi ya vituo vya nyuklia vya Iran.
-
Spika wa Baraza la Hamas apongeza mchango wa Iran katika kuwatetea Wapalestina
Jan 31, 2025 23:03Muhammad Ismail Darwish, Mwenyekiti wa Shura ya Hamas, ametoa shukurani kwa msaada na uungaji mkono wa Iran kwa watu wa Palestina, na kusema mchango wa Tehran ni muhimu katika mapambano yanayoendelea dhidi ya utawala wa ghasibu wa Israel.
-
Iran yaanza sherehe za Alfajiri Kumi za ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu
Jan 31, 2025 10:03Raia wa Iran leo wameanza sherehe za Alfajiri Kumi ili kuadhimisha mwaka wa 46 wa ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu yaliyouangusha utawala wa kifalme wa Pahlavi uliokuwa ukiungwa mkono na kusaidiwa na Marekani.
-
Hatibu wa Swala ya Ijumaa Tehran: Mafanikio muhimu ya Mapinduzi ya Kiislamu ni uzalishaji wa sayansi na elimu
Jan 31, 2025 10:00Imamu wa Swala ya Ijumaa ya leo mjini Tehran amesema: Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu anakutambua kuzalisha elimu na sayansi kuwa ndio njia ya kupata nguvu na kuwa imara, na mafanikio yenye thamani kubwa zaidi ya Mapinduzi ya Kiislamu ni uzalishaji wa sayansi na harakati ya kuelekea kwenye kilele cha elimu inaofanywa na vijana mahiri wa Iran.
-
Pezeshkian: Iran haijapokea ujumbe wowote kutoka Marekani
Jan 29, 2025 07:40Rais wa Iran Masoud Pezeshkian amesema kuwa Jamhuri ya Kiislamu haijapokea ujumbe wowote kutoka Washington hadi sasa.