-
Yemen: Israel inastahili kusambaratishwa na kufutwa katika eneo
Jan 05, 2023 03:30Balozi wa Yemen mjini Tehran amesema kila mtu ana jukumu na nafasi katika harakati ya muqawama, na jukumu lenyewe ni kutia nguvu jitihada za kuitimua Marekani katika eneo hili la Asia Magharibi, na kuufuta utawala haramu wa Israel katika eneo.
-
Netanyahu: Azimio la UN dhidi ya Israel halina umuhimu, linakirihisha
Jan 01, 2023 03:54Waziri Mkuu wa Israel amesema azimio jipya lililopitishwa dhidi ya utawala huo haramu katika Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa halina maana wala umuhimu wowote.
-
Israel yawaweka mamia ya watoto wa Kipalestina katika kifungo cha nyumbani
Dec 27, 2022 04:02Kamisheni ya Wafungwa wa Kipalestina imesema utawala haramu wa Israel umewaweka watoto zaidi ya 600 wa Kipalestina katika kifungo cha nyumbani, tokea mwanzoni mwa mwaka huu hadi sasa, huku utawala huo wa Kizayuni ukiendelea na kampeni yake ya kuwanyanyasa na kuwatia mbaroni Wapalestina.
-
Pigo jingine kwa Israel; Chile kufungua ubalozi wake Palestina
Dec 22, 2022 23:42Rais wa Chile, Gabriel Boric amesema nchi hiyo inapanga kufungua ubalozi wake huko Palestina kwa shabaha ya kuongeza kiwango cha uwakilishwaji wake rasmi katika taifa hilo linalokaliwa kwa mabavu na utawala wa Kizayuni wa Israel.
-
Muqawama: Tutalipiza kisasi cha mauaji ya Wapalestina Nablus
Dec 18, 2022 07:10Makundi ya muqawama ya Palestina yamelaani mauaji ya mandugu wawili wa Kipalestina katika mji wa Nablus, kaskazini mwa eneo la Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan linalokaliwa kwa mabavu na Wazayuni.
-
Israel yawakatia maji Wapalestina wa Ukingo wa Magharibi
Dec 15, 2022 22:55Utawala haramu wa Israel umewafungia maji mamia ya Wapalestina katika eneo la Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan.
-
Mbunge wa Kizayuni afichua: 2023 Saudia na Israel zitasaini mkataba wa kuanzisha uhusiano rasmi
Dec 13, 2022 22:56Mbunge wa chama cha Likud katika Bunge la utawala haramu wa Kizayuni wa Israel amesema, kwa kuzingatia mazungumzo yaliyofanyika, inatarajiwa kuwa makubaliano ya kuanzishwa uhusiano wa kawaida kati ya utawala huo na Saudi Arabia yatasainiwa mwaka ujao wa 2023.
-
Hamas: Wapalestina hawataiacha Israel itekeleze njama zake
Dec 12, 2022 23:24Mkuu wa ofisi ya kisiasa ya Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Palestina HAMAS amesema Wapalestina katu hawatouruhusu utawala haramu wa Israel utekeleza njama na mipango yake michafu dhidi ya mji mtakatifu wa Quds na Masjidul Aqsa.
-
Wazayuni wawashambulia Wapalestina wakisherehekea ushindi wa Morocco
Dec 11, 2022 07:40Jeshi katili la utawala wa Kizayuni wa Israel limewashambulia wananchi wa Palestina waliokuwa wamekusanyika kusherehekea ushindi wa Morocco katika mchuano wa robo fainali ya mechi za Kombe la Dunia zinazoendelea kushuhudiwa nchini Qatar.
-
Juhudi za Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa za kutokomeza silaha za nyuklia za Israel
Dec 11, 2022 05:29Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa limeanza kuchukua hatua kwa lengo la kutokomeza silaha za atomiki za utawala haramu wa Israel baada ya nchi 149 wanachama wa umoja huo kuunga mkono azimio linaloutaka utawala huo wa Kizayuni "uache kufuatilia uzalishaji, uundaji, majaribio au kutaka kuwa na silaha za nyuklia" na "kuachana na mpango wa kumiliki silaha za nyuklia".