-
Ivory Coast yataka kufanyika mkutano wa ECOWAS kujadili mzozo wa kidiplomasia na Mali
Sep 15, 2022 08:13Ivory Coast imeituhumu Mali kwa kuidai fidia na kuamiliana na wanajeshi wake 46 kama wahalifu baada ya kutiwa nguvuni na serikali ya Bamako. Serikali ya Ivory Coast imewaomba viongozi wa jumuiya ya Ecowas kujadili hali hiyo ya mgogoro kati yake na Bamako haraka iwezekanavyo.
-
Kiongozi wa Mali ataka 'fidia' ili kuwaachia askari wa Ivory Coast
Sep 11, 2022 12:00Rais wa mpito wa Mali amesema anataka suluhu yenye maslahi ya pande mbili ili kuhitimisha mkwaruzano wa kidiplomasia baina ya nchi hiyo na Ivory Coast.
-
Mali yawaachia askari watatu wa Ivory Coast, 46 wangali wako kizuizini
Sep 04, 2022 10:37Mali imewaachia huru askari watatu wanawake kati ya askari 49 wa Ivory Cooast waliokamatwa na kuwekwa kizuizini nchini humo.
-
Mali: Wanajeshi wa Ivory Coast waliotuhumiwa kuwa 'mamluki' wameshtakiwa na kufungwa
Aug 16, 2022 02:43Duru za mahakama nchini Mali zimeripoti kuwa, wanajeshi 49 wa Ivory Coast waliozuiliwa kwa zaidi ya mwezi mmoja katika mji mkuu Bamako, wakishutumiwa na jeshi lililoko madarakani nchini Mali kwa kuwa "mamluki", madai ambayo serikali ya Abidjan inakanusha, wameshtakiwa kwa "kujaribu kuhatarisha usalama wa taifa" na kuhukumiwa kifungo jela.
-
Rais wa Ivory Coast atoa msamaha kwa mtangulizi wake, Laurent Gbagbo
Aug 07, 2022 12:36Rais Alassane Ouattara wa Ivory Coast ametoa msamaha kwa mtangulizi wake, mshindani wake mkuu na hasimu wake wa muda mrefu Laurent Gbagbo, ikiwa ni sehemu ya kuleta maridhiano nchini kuelekea uchaguzi mkuu unaotazamiwa kufanyika 2025.
-
Mali yamtimua msemaji wa kikosi cha UN nchini humo, MINUSMA
Jul 21, 2022 11:01Mali imemfukuza msemaji wa kikosi cha kulinda amani cha Umoja wa Mataifa nchini humo (MINUSMA), huku uhusiano baina ya Bamako na UN ukizidi kuharibika.
-
Ivory Coast yaitaka Mali kuwaachilia huru wanajeshi 49 waliokamatwa Bamako
Jul 14, 2022 03:17Ivory Coast imetaka kuachiliwa huru wanajeshi wake 49 waliokamatwa nchini Mali, tukio ambalo huenda likazidisha mvutano kati ya watawala wa kijeshi wa Mali na mataifa mengine ya Magharibi mwa Afrika huku kukiwa na juhudi za kuzima harakati za makundi yenye silaha yenye uhusiano na al-Qaida na Daesh (ISIS) na kurejesha utawala wa kidemokrasia nchini humo.
-
Kodivaa; mwenyeji wa mkutano wa COP15 wa kuzuia kuenea majangwa duniani
May 10, 2022 04:26Mkutano wa 15 wa kuzuia kuenea majangwa umeanza shughuli zake huko Abdijan mji mku uwa Kodivaa kwa kuhudhuriwa na viongozi wa nchi mbalimbali za Kiafrika na wa nchi nyingine duniani.
-
Watu 11 waugua homa ya Dengi (Dengue) Kodivaa
May 04, 2022 08:09Wizara ya Afya ya Kodivaa imetangaza kuwa, kesi 11 za homa ya Dengue zimeripotiwa nchini humo; akthari zikiwa Abidjan mji mkuu wa zamani wa nchi hiyo.
-
Ivory Coast yarekodi kisa cha kwanza cha Ebola katika miaka 25
Aug 15, 2021 13:28Waziri wa Afya wa Ivory Coast ametangaza kuwa nchi hiyo imesajili kisa cha kwanza cha virusi vya kutokwa na damu vya Ebola ikiwa ni mara ya kwanza katika kipindi cha miaka 25.