Kodivaa; mwenyeji wa mkutano wa COP15 wa kuzuia kuenea majangwa duniani
(last modified Tue, 10 May 2022 04:26:38 GMT )
May 10, 2022 04:26 UTC
  • Kodivaa; mwenyeji wa mkutano wa COP15 wa kuzuia kuenea majangwa duniani

Mkutano wa 15 wa kuzuia kuenea majangwa umeanza shughuli zake huko Abdijan mji mku uwa Kodivaa kwa kuhudhuriwa na viongozi wa nchi mbalimbali za Kiafrika na wa nchi nyingine duniani.

Mkutano huo wa COP15 wa kuzuia kuenea majangwa duniani utatoa kipaumbele na kuzingatia pakubwa suala la kuhuisha hekari bilioni moja za ardhi iliyoharibiwa hadi kufikia mwaka 2030, matumizi endelevu ya ardhi katika kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi na kukabiliana na ongezeko la hatari za majanga ya kimaumbile kama ukame, kuongezeka kwa uchaguzi wa hali ya hewa, dhoruba, vimbunga vya vumbi na moto wa misituni.   

Lengo la mkutano huo wa COP15 ambao ulianza jana huko Kodivaa ni kutekelezwa juhudi za kukabiliana na kuharibiwa haraka ardhi na taathira zake mbaya kwa viumbe hai na binadamu. 

Kuenea hali ya majangwa barani Afrika 

Viongozi wa nchi 9 za Kiafrika wakiwemo Marais Mohamed Bazoum wa Niger, Felix Tshisekedi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Faure Gnassingbe wa Togo na Alassane Ouatara wa Kodivaa wanashiriki mkutano huo. 

Rais Emmanuel Macron wa Ufaransa na Mkuu wa Kamisheni ya Ulaya Ursula Von derline pia wameshiriki mkutano huo kwa njia ya intaneti. Washiriki katika Mkutano wa COP15 huko Abdijan wanataraji kufikia mapatano kwa kuainisha hatua zinazofaa ili kuzuia kuongezeka majangwa duniani.