Iran yasambaratisha mtandao wa mamluki wa Marekani na Israel
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i133122-iran_yasambaratisha_mtandao_wa_mamluki_wa_marekani_na_israel
Kikosi cha Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran SEPAH kimesambaratisha mtandao wa kijasusi hapa nchini uliokuwa ukiendesha harakati za kuvuruga usalama na amani.
(last modified 2025-11-16T06:33:27+00:00 )
Nov 13, 2025 07:21 UTC
  • Jeshi la SEPAH latangaza kusambaratisha mtandao wa mamluki wa Marekani na Israel
    Jeshi la SEPAH latangaza kusambaratisha mtandao wa mamluki wa Marekani na Israel

Kikosi cha Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran SEPAH kimesambaratisha mtandao wa kijasusi hapa nchini uliokuwa ukiendesha harakati za kuvuruga usalama na amani.

Kitengo cha Kiintelijensia cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu kimetangaza kuwa, kimefanikiwa kutambua na kuharibu mtandao wa kuvuruga usalama uliokuwa ukiongozwa na mashirika ya kijasusi za Marekani na utawala ghasibu wa Israel ndani ya Iran.

Taarifa ya SEPAH imesema: Tunapenda kuwafamaisha wananchi wapen wa wa Iran kwamba, kupitia hatua zilizochukuliwa na Idara ya Intelijensia ya Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (SEPAH), mtandao wa kuvuruga amani na usalama uliokuwa ukiongozwa na mashirika ya kijasusi ya Marekani na Israel ulitambuliwa ndani ya nchi na kusambaratishwa baada ya duru kadhaa za ufuatiliaji na hatua nyingine za kijasusi.

Sehemu nyingine ya taarifa hiyo imesema: Utawala wa Kizayuni ukiwa kikosi kiwakilishi cha Marekani katika eneola Asia Magharibi baada ya kushindwa katika Vita vya Siku 12, umebadilisha sera na mipango yake kuelekea kuvuruga usalama wa umma, kwa matumaini kwamba, pengine utaweza kufidia kushindwa kwake kwa kufedhehesha katika medani ya kijeshi.

Hayo yanajiri katika hali ambayo, hivi majuzi jeshi la SEPAH lilitangaza mafanikio makubwa ya kukabiliana na ujasusi, baada ya kumkamata kiongozi wa kundi la udukuzi linalojulikana kama "Backdoor."

kiongozi wa kundi hilo alifanya kazi kwa kutumia jina bandia la msichana Mholanzi akidai kutetea uhuru wa wanawake wa Iran, na inasemekana alikuwa akitoa taarifa za siri kuhusu vikosi vya usalama vya Iran kwa mitandao ya vyombo vya habari vinavyopinga Jamhuri ya Kiislamu, ikiwa ni pamoja na Iran International, na mitandao iliyounganishwa na shirika la ujasusi la Israel, Mossad.