Iran yamkamata jasusi mkongwe wa Mossad na magaidi katika operesheni za kitaifa
Wizara ya Usalama wa Taifa Iran imetangaza kukamatwa kwa jasusi “mzoefu” aliyekuwa akifanya kazi kwa niaba ya utawala wa Kizayuni wa Israel, pamoja na wanachama 15 wa makundi ya kigaidi ya makundi ya wanaotaka kujitenga, kufuatia operesheni zilizofanyika katika mikoa mbalimbali nchini
Kwa mujibu wa taarifa, katika Mkoa wa Ilam, jasusi mkongwe wa shirika la kijasusi la Israel, Mossad , alinaswa baada ya kukusanya na kutuma taarifa za kiusalama kwa shirika la ujasusi la adui Mzayuni, na baadaye , kwa maelekezo ya kinanrai wake — kuanza kushirikiana na makundi ya ya upinzani ya wanaounga mkonoufalme wa kiimla uliopinduliwa
Katika Mkoa wa Sistan na Baluchestan, mwanachama wa operesheni katika kundi moja la kigaidi la kujitenga alikamatwa. Imedokezwa kuwa alipata mafunzo katika nchi jirani kabla ya kuingia Iran kwa lengo la kufanya mashambulizi karibu na mji wa Zahedan.
Katika Mkoa wa Gilan, seli ya magaidi watatu ilikamatwa, na kifaa cha kurushia mabomu ya kutengenezwa nyumbani kilipatikana kwenye maficho yao.
Katika Mkoa wa Lorestan, kundi la watu wawili wanaume na mwanamke mmoja lilinaswa. Walikuwa wamepokea malipo kwa njia ya sarafu ya kidijitali na walikuwa wametengeneza mabomu kadhaa kwa lengo la kushambulia ofisi za magavana wa wilaya mbili.
Katika Mkoa wa Azarbaijan ya Magharibi, watu tisa wanaodaiwa kuhusishwa na makundi ya kigaidi ya kujitenga walikamatwa walipokuwa wakipanga mashambulizi yanayodaiwa kuendana na mipango ya maadui wanaoungwa mkono na Marekani na Israel.
Kwa upande mwingine, Shirika la Usalama la Jeshi la Iran la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) lilitangaza Jumamosi pia kuwa limebaini na kuvunja timu kadhaa zinazohusishwa na makundi ya kupinga mapinduzi yaliyokuwa yakifanya kazi katika mikoa ya Kurdistan na Kermanshah.
IRGC imesema timu hizo zilikuwa zikisaidiwa na Marekani na utawala wa Kizayuni, na zilikuwa zikijaribu kuandaa mazingira ya shambulio la kijeshi la adui dhidi ya Iran kutoka upande wa magharibi.
Hatua hizi za kiusalama zimekuja kufuatia vita vya kichokozi vya Marekani na Israel dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu, vilivyoanza Februari 28 na kuendelea kwa siku 40.
Vyombo vya usalama vya taifa vimeripoti kuwakamata watu wengi waliohusika katika njama za kuvuruga amani, huku Majeshi ya Jamhuri ya Kiislamu yakikabiliana na wavamizi kupitia mashambulizi dhidi ya ngome za Marekani na Israel katika eneo la Asia Magharibi.