-
Hatua mpya za vikwazo vya Marekani dhidi ya Iran
Jun 11, 2021 08:25Wizara ya Biashara ya Marekani Alkhamisi ya jana iliwaweka watu na mashirika kadhaa katika orodha yake ya vikwazo kwa kisingizio cha nafasi yao katika kudhamini fedha kwa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (Sepah) na harakati ya wapiganaji wa kujitolea ya Ansarullah nchini Yemen.
-
Zarif amjibu Blinken: Nenda usome kipengee cha 36 cha mkubaliano ya nyuklia ya JCPOA
Jun 08, 2021 11:15Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amejibu madai ya waziri mwenzake wa mambo ya Nje wa Marekani aliyedai kuwa, haijulikani kwamba Iran ina hamu au iko tayari kurejea kwenye mapatano ya nyuklia ya JCPOA. Muhammad Javad Zarif amemwambia Blanken kwamba: Inakutosha usome kipengee cha 36 cha JCPOA.
-
Ujerumani: Mazungumzo ya JCPOA yapo katika hatua za mwisho
Jun 07, 2021 22:01Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani amesema mazungumzo kuhusu makubaliano ya nyuklia ya JCPOA yanayoendelea huko Vienna, Austria yapo katika kipindi cha lala salama.
-
BRICS yataka kutekelezwa kikamilifu Azimio 2231 la Baraza la Usalama la UN
Jun 02, 2021 03:27Nchi wanachama wa kundi la BRICS zimetoa mwito wa kupatia ufumbuzi kadhia ya nyuklia ya Iran kwa njia ya amani; huku zikisisitizia udharura wa kutekelezwa kikamilifu Azimio Nambari 2231 la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.
-
Umoja wa Ulaya wakaribisha kurefushwa makubaliano ya kiufundi kati ya Iran na IAEA
May 26, 2021 03:59Enrique Mora Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Ulaya Kuhusu Hatua za Kigeni amekaribisha makubaliano ya kiufundi yaliyofikiwa hivi karibuni kati ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Nyuklia IAEA na kuyataja kuwa 'makuabaliano mazuri.' Amesema makubaliano hayo yataandaa uwanja unaofaa kwa ajili ya kufikiwa mapatano ya kuridhisha mjini Vienna.
-
Araqchi: Mapatano yamefikiwa kuhusu kuondolewa asilimia 95 ya vikwazo
May 23, 2021 21:59Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amesema kuwa mapatano yamefikiwa kuhusu kuondolewa asilimia 95 ya vikwazo.
-
Mwaka wa tatu wa Marekani kujitoa katika mapatano ya JCPOA, juhudi nyingi zisizo na maana
May 09, 2021 21:04Miaka mitatu iliyopita, Mei 8 2018, Donald Trump rais wa zamani wa Marekani aliiondoa rasmi nchi hiyo katika mapatano ya kimataifa ya nyuklia mashuhuri kama JCPOA, kwa madai kwamba yalikuwa mapatano mabaya zaidi kuwahi kufikiwa katika historia ya nchi hiyo.
-
Zarif aonesha hisia zake kufuatia miaka mitatu ya kujitoa Marekani katika JCPOA
May 09, 2021 01:29Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ameonesha hisia zake kufuatia miaka mitatu ya kujitoa Marekani katika mapatano ya nyuklia ya JCPOA na kuandika katika ukurasa wake wa Twitter kwamba miaka mitatu iliyopita, kulizuka "kinyago cheusi" katika ahadi za Marekani ndani ya ndani ya azimio nambari 2231 na mapatano ya JCPOA baada ya Marekani kujitoa katika makubaliano hayo.
-
Araqchi: Kumefikiwa mapatano ya kuondoa aghalabu ya vikwazo dhidi ya Iran
May 02, 2021 03:06Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ameashiria kikao cha jana cha Tume ya Pamoja ya Mapatano ya Nyuklia ya JCPOA na kusema kikao hicho kimefikia mwafaka kuhusu kuondolewa Iran vikwazo.
-
Putin ataka kuhuishwa JCPOA katika muundo wake wa asili
May 01, 2021 08:46Rais Vladmir Putin wa Russia ametoa mwito wa kuhuishwa makubaliano ya nyuklia ya JCPOA na kuyarejesha katika muundo wake wa asili.