Putin ataka kuhuishwa JCPOA katika muundo wake wa asili
(last modified Sat, 01 May 2021 13:16:03 GMT )
May 01, 2021 13:16 UTC
  • Putin ataka kuhuishwa JCPOA katika muundo wake wa asili

Rais Vladmir Putin wa Russia ametoa mwito wa kuhuishwa makubaliano ya nyuklia ya JCPOA na kuyarejesha katika muundo wake wa asili.

Rais Putin ametoa mwito huo katika hotuba yake kwa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, ambapo ameashiria kuhusu maudhui kadhaa zinazojadiliwa hivi sasa katika kikao cha Kamisheni ya Pamoja ya makubaliano ya JCPOA kinachofanyika huko Vienna, Austria.

Amesema, "natumai kila kitu kinachohusiana na JCPOA kitarejea katika hali yake ya mwanzo, na tutaweza kujenga mahusiano na washiriki wote wa eneo la Caspian, na vile vile tutaweza kutekeleza mipango yetu."

Rais Putin ameitaja Iran kama jirani mwema katika eneo la Bahari ya Caspian na kusisitiza kuwa, kufufuliwa JCPOA kutaisaidia Moscow kupanua zaidi uhusiano wake na Jamhuri ya Kiislamu na nchi nyingine za eneo.

Mazungumzo ya JCPOA

Rais wa Russia amesema hayo katika hali ambayo,  duru zinasema kuwa, licha ya kuwa mazungumzo hayo ya Vienna kuwa magumu lakini kumepigwa hatua nzuri na kwamba, pande husika zimo katika mchakato wa kuandaa muswada wa mapatano.

Jamhuri ya Kiislamu ya Iran inasisitiza kuwa, vikwazo vyote vilivyowekwa na Marekani baada ya kusainiwa makubaliano ya nyuklia ya JCPOA mwaka 2015, sawa viwe vimewekwa katika kipindi cha utawala wa Barack Obama au kipindi cha utawala wa Donald Trump vinapaswa kuondolewa, ili Tehran ianze kutekeleza tena kikamilifu vipengee vya mapatano hayo.

Tags