Ufaransa yatangaza kuwa tayari kutuma wanajeshi nchini Ukraine
https://parstoday.ir/sw/news/daily_news-i132434-ufaransa_yatangaza_kuwa_tayari_kutuma_wanajeshi_nchini_ukraine
Pars Today- Mkuu wa Komandi Kuu ya Jeshi la Ufaransa ametangaza kwamba ikiwa Russia na Ukraine zitafikia makubaliano ya kusitisha mapigano, Paris itakuwa tayari kutuma wanajeshi nchini Ukraine kama sehemu ya kutoa dhamana za usalama kutoka kwa nchi za Magharibi.
(last modified 2025-10-26T11:24:27+00:00 )
Oct 26, 2025 10:19 UTC
  • Ufaransa yatangaza kuwa tayari kutuma wanajeshi nchini Ukraine

Pars Today- Mkuu wa Komandi Kuu ya Jeshi la Ufaransa ametangaza kwamba ikiwa Russia na Ukraine zitafikia makubaliano ya kusitisha mapigano, Paris itakuwa tayari kutuma wanajeshi nchini Ukraine kama sehemu ya kutoa dhamana za usalama kutoka kwa nchi za Magharibi.

Jenerali Pierre Schill amesema kwamba Paris iko tayari kutuma wanajeshi kuiunga mkono Ukraine kama sehemu ya dhamana za usalama za nchi za Magharibi kwa Kyiv.

Schill amesema hayo wakati akizungumza kwenye mkutano wa Kamati ya Ulinzi ya Bunge la Ufaransa na kuongeza kwamba, jeshi la Ufaransa limewekwa katika hali ya "dharura ya kitaifa" na kwamba wanajeshi elfu saba tayari wako kwenye hali ya kutumika wakati wowote wanapohitajika.

Taarifa hizo zimetolewa wakati ambapo huko nyuma kamanda huyo wa vikosi vya jeshi la Ufaransa alikuwa amesema kwamba kuna uwezekano wa kuzuka mzozo mpya kati ya Ulaya na Russia, hasa baada ya Moscow kuonya dhidi ya mpango wa nchi za Magharibi kupeleka vikosi vya NATO nchini Ukraine.

Kwa hisani ya shirika la habari la Mehr