-
John Kerry: JCPOA ni mapatano bora kabisa katika uso wa dunia
Nov 17, 2018 13:00Waziri wa zamani wa mambo ya nje wa Marekani ametetea mapatano ya nyuklia ya Iran maarufu kwa jina la JCPOA na kusema kuwa makubaliano hayo ni mapatano imara zaidi, makini zaidi, ya wazi zaidi na yaliyozingatia pande zote zaidi kabla ya kufikiwa kwake.
-
IAEA yathibitisha kwa mara ya 13: Iran inatekeleza kikamilifu JCPOA
Nov 13, 2018 00:29Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki umetoa ripoti yake mpya ya msimu na kuthibitisha kwa mara ya 13 kuwa Iran ingali inatekeleza ahadi na majukumu yake yote katika makubaliano ya nyuklia ya JCPOA.
-
Hatua za mwisho za Ulaya za kuanzisha mfumo huru maalumu wa kifedha kati yake na Iran
Nov 03, 2018 23:05Kufuatia kutangazwa duru mpya ya vikwazo vya Marekani dhidi ya Iran ambavyo vinatazamiwa kuanza kutekelezwa kuanzia tarehe 5 mwezi huu huku vikijumuisha sekta ya mafuta, benki na safari za meli; nchi za Ulaya zimetoa taarifa zikisisitiza kupiga hatua kubwa katika kutayarisha mfumo huo maalumu wa kifedha kati yake na Iran.
-
Rouhani: Nchi za Ulaya zikabiliane na Marekani kwa kushirikiana na Iran
Nov 02, 2018 02:38Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa sera za Marekani zimehatarisha uthabiti katika uga wa kimataifa na hivyo ametoa wito kwa nchi za Ulaya kushirikiana na Iran katika kukabiliana na maamuzi ya upande moja ya watawala wa Washington.
-
Umoja wa Ulaya: Uungaji mkono wetu kwa makubaliano ya JCPOA uko pale pale
Oct 31, 2018 21:53Umoja wa Ulaya umejibu tuhuma za hivi karibuni za Denmark dhidi ya Iran kwa kusema: Brussels inasubiri taarifa zaidi kutoka Copenhagen kuhusu suala hilo na kwamba uungaji mkono wa umoja huo kwa makubaliano ya JCPOA uko pale pale.
-
Ulaya yakerwa na vikwazo vya Marekani dhidi ya Iran na kusisitiza kulindwa mapatano ya JCPOA
Oct 30, 2018 22:50Rais Donald Trump wa Marekani daima amekuwa akijaribu kuvuruga mapatano ya kimataifa yaliyofikiwa kati ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na kundi la 5+1 kwa kisingizio kuwa ni mapatano mabaya zaidi ya kimataifa kuwahi kufikiwa na Marekani.
-
Ulaya na Umoja wa Mataifa zasisitiza azma yao ya kuyalinda makubaliano ya JCPOA
Oct 25, 2018 08:28Licha ya Marekani kuyapinga makubaliano ya nyuklia ya JCPOA, lakini nchi za Ulaya zinasisitiza kulindwa makubaliano hayo muhimu ya kimataifa. Rais Donald Trump wa Marekani amekuwa akichukua misimamo iliyo dhidi ya makubaliano hayo ambayo yalifikiwa mwezi Julai mwaka 2015 kati ya Iran na kundi la 5+1 ikiwemo marekani yenyewe na anayataja kuwa ni makubaliano mabaya zaidi kuwahi kufikiwa!
-
Uungaji mkono wa wakuu wa nchi za Asia na Ulaya kwa makubaliano ya JCPOA
Oct 20, 2018 08:31Japokuwa Marekani ni miongoni mwa nchi sita ambazo zilifikia makubaliano ya nyuklia na Iran katika kalibu ya nchi zinazounda kundi la 5+1 mwezi Januari mwaka 2015 lakini Rais Donald Trump wa nchi hiyo ameonekana akichukua msimamo wa kuyapinga makubaliano hayo; huku akiyataja kuwa ni makubaliano mabaya zaidi kuwahi kufikiwa.
-
Uingereza: Kufungamana na JCPOA ni msingi wa uhusiano wetu na Iran
Oct 14, 2018 04:21Balozi wa Uingereza nchini Iran amesema kufungamana na makubaliano ya nyuklia ya JCPOA kama mapatano ya kimataifa ni msingi wa uhusiano wa London na Tehran.
-
Sisitizo la Russia na India la kutekelezwa kikamilifu mapatano ya nyuklia ya JCPOA
Oct 07, 2018 23:03India na Russia wakiwa wanachama wa kundi la BRICS ambao wanataka mabadiliko katika muundo wa kimataifa utakao kuwa mbali na udhibiti wa Magharibi hususan Marekani, zimetangaza tena uungaji mkono wao kwa mapatano ya nyuklia ya JCPOA.