Uingereza: Kufungamana na JCPOA ni msingi wa uhusiano wetu na Iran
(last modified Sun, 14 Oct 2018 07:51:55 GMT )
Oct 14, 2018 07:51 UTC
  • Uingereza: Kufungamana na JCPOA ni msingi wa uhusiano wetu na Iran

Balozi wa Uingereza nchini Iran amesema kufungamana na makubaliano ya nyuklia ya JCPOA kama mapatano ya kimataifa ni msingi wa uhusiano wa London na Tehran.

Rob Macaire ameyasema hayo katika mkutano wake na Gavana wa Mkoa wa Fars hapa nchini, Ismail Tabadar na kuongeza kuwa, Uingereza inafanya juu chini kuhakikisha kuwa Iran inastafidi na mapatano hayo hususan katika uga wa uchumi.

Amesema kuimarisha uhusiano wa kibiashara na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na hususan katika mahitaji ya msingi kama chakula, dawa na huduma za afya kunapaswa kuwa hatua ya kwanza ya kupanua uhusiano wa pande mbili wa London na Tehran.

Kwa upande wake, Gavana wa mkoa wa Fars, kusini magharibi mwa Iran amesema daima Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imekuwa ikinyoosha mkono wa udugu kwa mataifa mengine kama vile Uingereza, na kusisitiza kuwa nchi za Ulaya zina wajibu wa kushikamana kikamilifu na makubaliano ya nyuklia ya Vienna.

Balozi wa Uingereza Tehran alipokutana na Rais Hassan Rouhani miezi 2 iliyopita

Trump tarehe 8 Mei mwaka huu alitangaza habari ya kujiondoa Marekani katika makubaliano hayo ya nyuklia na kuiwekea tena Iran vikwazo vya nyuklia.

Umoja wa Ulaya ambao nchi zake 3 zinazounda Troika ya Ulaya yaani Ujerumani, Ufaransa na Uingereza ambazo ni wananchama wa kundi la 5+1, unaunga mkono makubaliano hayo ya nyuklia na kusisitiza udharura wa kukabiliana na hatua za Marekani za kutaka kuyafuta. 

Tags