-
Wasichana wahajiri wa Kiafrika wananajisiwa na hata kupewa ujauzito katika kambi ya EU, Libya
Jun 21, 2021 12:42Kundi la wasichana wahamiaji waliowekwa katika kituo kinachosimamiwa na serikali ya Libya wamewashutumu walinzi wa kituo hicho, kinachofadhiliwa na Umoja wa Ulaya, kwamba wanawabaka na kuwanyanyasa kingono.
-
UN: Kundi la Daesh lilifanya jitihada za kuangamiza Waislamu wa madhehebu ya Shia
May 12, 2021 00:47Mkuu wa timu ya Umoja wa Mataifa iliyopewa jukumu la kuchunguza jinai na uhalifu uliofanywa na kundi la kiwahabi la Daesh amesema kuwa, kundi hilo la kigaidi lilifanya jitihada za kuangamiza Waislamu wa madhehebu ya Shia.
-
Foreign Policy yafichua taasisi bandia inayodai kuwa na uhusiano na UN, inahusishwa na uhalifu wa kimataifa
Mar 25, 2021 02:34Uchunguzi uliofanywa na gazeti la Foreign Policy umefichua habari za taasisi moja inayodai kuwa na uhusiano na Umoja wa Mataifa na kutetea haki za binadamu ambayo viongozi wake wanatuhumiwa kuhusika na uhalifu na jinai nyingi zikiwemo za kutakatisha fedha chafu na kutorosha mabilioni ya dola za Marekani zilizokuwa zimeporwa kutoroshwa nje ya nchi na kiongozi wa zamani wa Libya, Muammar Gaddafi kabla ya kuuawa kwake.
-
Waziri wa Polisi Afrika Kusini: Uhalifu “umeenda likizo” katika kipindi cha maambukizi ya corona
Aug 15, 2020 10:39Takwimu zinaonesha kuwa kesi za visa vya uhalifu, katika nchi iliyoathiriwa sana na kiwango cha juu cha jinai na uhalifu ya Afrika Kusini, zimepungua sana katika kipindi cha miezi mitatu ya kwanza ya utekelezaji wa sheria kali za kupambana na maambukizi ya virusi vya corona nchini humo.
-
Uturuki: Imarati imefanya jinai za kivita na mauaji ya kimbari huko Yemen
Jul 03, 2020 09:46Mwakilishi wa kudumu Uturuki katika Umoja wa Mataifa amesema kuwa serikali ya Umoja wa Falme za Kiarabu (Imarati) imefanya jinai za kivita na mauaji ya kimbari katika vita vya Yemen.
-
Mahakama ya Kimataifa ya Jinai yamkamata kiongozi wa Janjaweed
Jun 10, 2020 05:24Mahakama ya Kimataifa ya Jinai (ICC) imetangaza kuwa, kiongozi wa wanamgambo wa Janjaweed Ali Kosheib ambaye alikuwa mtu wa karibu kwa rais wa zamani wa Sudan, Omar al Bashir amejisalimisha kwa mahakama hiyo na kwamba anakabiliwa na tuhuma za kutenda jinai za kivita katika jimbo la Darfur huko magharibi mwa Sudan tangu mwaka 2003.
-
Maafisa wa Imarati wafunguliwa mashtaka ya kufanya uhalifu wa kivita huko Yemen
Feb 13, 2020 11:28Shirika moja la mawakili la Uingereza limefungua mashtaka dhidi ya maafisa wa serikali ya Imarati kwa tuhuma za kutenda jinai za kivita nchini Yemen.
-
Serikali ya Sudan na wapinzani wa Darfur wakubaliana kuwakabidhi watenda jinai kwa mahakama ya ICC
Feb 12, 2020 02:58Serikali ya Sudan na viongozi wa makundi ya upinzani katika eneo la Darfur wamefikia makubaliano ya kuwakabidhi watenda jinai za kivita katika eneo hilo lililoko magharibi mwa Sudan kwa Mahakama ya Kimataifa ya Jinai (ICC) akiwemo rais wa zamani wa nchi hiyo, Omar al Bashir.
-
Serikali ya Sudan yatwaa mali za chama cha rais wa zamani wa nchi hiyo, al Bashir
Jan 09, 2020 08:02Serikali ya Sudan imetwaa mali za chama kilichovunjwa cha rais wa zamani wa nchi hiyo, Omar al Bashir kilichovunjwa na kupigwa marufuku nchini humo.
-
Ripoti: Wasudani hawaridhishwi na hukumu iliyotolewa dhidi ya Omar al Bashir
Dec 15, 2019 13:27Vyombo vya habari vimeripoti kuwa, wananchi wa Sudan hawakuridhishwa na hukumu ya kifungo cha miaka miwili katika kituo cha marekebisho ya kitabia iliyotolewa dhidi ya kiongozi aliyeondolewa madarakani wa nchi hiyo, Omar al Bashir, baada ya kupatikana na hatia ya ubadhirifu wa fedha za umma na ufisadi.