-
Suu Kyi afunguliwa mashtaka kwa mara ya kwanza kwa jinai dhidi ya Wislamu wa Myanmar
Nov 15, 2019 01:24Makundi ya kutetea haki za binadamu huko Amerika ya Latini yamewasilisha kesi dhidi ya Aung San Suu Kyi Mshauri wa ngazi ya juu wa serikali ya Myanmar na maafisa wa ngazi za juu wa jeshi la nchi hiyo kwa tuhuma za kuhusika na jinai na uhalifu uliofadhiliwa na serikali ya nchi hiyo dhidi ya Waislamu wa kabila la waliochache la Rohingya.
-
Ntaganda ahukumiwa kifungo cha miaka 30 jela kwa kutenda jinai za kivita Congo DR
Nov 07, 2019 13:32Mahakama ya Kimataifa ya Jinai (ICC) imemhukumu kifungo cha miaka 30 jela mbabe wa zamani wa vita katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Bosco Ntaganda baada ya kumpata na hatia ya kufanya ukatili ikiwa ni pamoja na kuua, kubaka na kuwatumikisha watoto kama askari vitani.
-
UN: Mashambulizi ya Marekani nchini Syria ni sawa na jinai za kivita
Sep 12, 2019 07:54Umoja wa Mataifa umetangaza kuwa, mashambulizi yanayofanywa na Marekani na washirika wake huko Syria ni sawa na jinai za kivita.
-
Ripoti ya UN: Marekani, Uingereza na Ufaransa zinahusika kutenda jinai za kivita nchini Yemen
Sep 04, 2019 12:40Wachunguzi wa Umoja wa Mataifa wameandaa orodha ya siri ya watuhumiwa wa kimataifa waliohusika na jinai za kivita nchini Yemen inayoonyesha kuwa Marekani na nchi kadhaa za Ulaya zimehusika pia katika jinai hizo kwa kuuzuia silaha muungano vamizi wa kijeshi unaoongozwa na Saudi Arabia.
-
Shirika la Haki za Binadamu Barani Ulaya: Uhalifu wa Israel dhidi ya Palestina ni jinai za kivita
Jul 10, 2019 02:32Shirika la Haki za Binadamu Barani Ulaya na Mediterania limetangaza kuwa, uhalifu unaofanywa na Israel dhidi ya haki za Wapalestina ni jinai za kivita na kuna haja ya kuwepo usimamizi makhsusi wa kufuatilia jinai hizo.
-
Answarullah: Nchi zinazoishambulia Yemen zinatekeleza jinai zilizoratibiwa kimataifa
Jun 09, 2019 03:06Harakati ya Answarullah ya nchini Yemen imetoa radiamali yake kufuatia shambulizi la vibaraka wa Imarati dhidi ya Waislamu waliokuwa wanaswali msikitini katika mkoa wa Ad Dali na kusema kuwa, jinai hiyo ni moja ya jinai zilizoratibiwa kimataifa.
-
Radiamali ya Donald Trump kwa uamuzi wa Mahakama ya Kimataifa ya Jinai ICC
Apr 14, 2019 08:02Rais Donald Trump wa Marekani ambaye alishika hatamu za uongozi wa nchi hiyo Januari mwaka 2017, ameamua kuchukua mkondo wa kupuuza, kukosoa na kujiondoa katika asasi na jumuiya za kimataifa.
-
Madai ya Muungano wa Kimarekani ya eti kupambana na ugaidi, urongo mkubwa wa karne
Mar 19, 2019 03:06Serikali ya Syria imeutuhumu muungano eti wa kimataifa wa kupambana na Daesh unaoongozwa na Marekani kuwa umefanya jinai za kivita.
-
Pompeo: Marekani itawanyima viza majaji wa mahakama ya ICC
Mar 16, 2019 04:43Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani amesema kuwa, nchi hiyo itawawekea marufuku ya viza ya kuingia Marekani maafisa wa Mahakama ya Kimataifa ya Jinai watakaotaka kuwasaili na kuwachunguza wanajeshi wa nchi hiyo wanaotuhumiwa kufanya jinai za kivita huko Afghanistan.
-
Jumuiya ya Nchi za Kiarabu yaunga mkono ripoti ya UN kuhusu jinai za Israel
Mar 01, 2019 08:13Jumuiya ya Nchi za Kiarabu, Arab League, imeunga mkono ripoti ya hivi karibuni ya Umoja wa Mataifa kuhusu jinai ambazo zinatendwa na utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya Wapalestina katika Ukanda wa Ghaza.