-
Shughuli ya kuuaga mwili wa shahidi Luteni Jenerali Qassem Soleimani yafanyika Kadhimain, Iraq
Jan 04, 2020 07:16Shughuli maalumu ya maombolezo ya kuuaga mwili wa shahidi Qassem Soleimani, kamanda wa kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) pamoja na wanamapambano wenzake waliouawa shahidi pamoja naye imefanyika katika mji wa Kadhimain nchini Iraq.
-
Nchi Kadhaa Duniani zalaani mauaji ya Qassem Soleimani
Jan 04, 2020 02:40Nchi kadhaa duniani zimeilaani vikali Marekani kwa kumuua kigaidi Luteni Jenerali Qassem Soleimani, Kamanda wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu.
-
Sayyid Nasrullah: Vikosi vya Muqawama kote duniani kujibu mapigo ya kuuawa shahidi Soleimani
Jan 03, 2020 13:55Katibu Mkuu wa harakati ya Hizbullah ya Lebanon amesema vikosi vya wanamuqawama kote duniani vina jukumu la kuwaadhibu wale waliohusika na mauaji ya kikatili ya Kamanda wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu, Meja Jenerali Qassem Solaimani.
-
Wairani waandamana kote nchini kuomboleza mauaji ya Jen. Soleimani
Jan 03, 2020 12:32Wananchi wa Iran katika mikoa na miji mbalimbali ukiwemo mji mkuu Tehran wamemiminika mabarabarani baada ya Sala ya Ijumaa kushiriki maandamano ya kuomboleza na kulaani mauaji ya kamanda wa ngazi za juu wa Jeshi la Iran.
-
Bei za mafuta na dhahabu zapanda duniani kufuatia mauaji ya Jenerali Soleimani
Jan 03, 2020 12:15Bei za mafuta na dhahabu katika soko la kimataifa kote duniani zimepanda kufuatia kuuliwa shahidi Kamanda wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu la Iran, Meja Jenerali Qassem Soleimani.
-
Kuuawa shahidi Meja Jenerali Qassim Solaimani; mfano wa wazi wa jinai za kivita za Marekani
Jan 03, 2020 11:53Meja Jenerali Qassim Solaimani, Kamanda wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (SEPAH) na Abu Mahdi al Muhandes, Naibu Mkuu wa Kikosi cha Kujitolea cha Wananchi wa Iraq cha al-Hashdul al-Shaabi, wameuawa shahidi usiku wa kuamkia Ijumaa ya leo katika shambulio la roketi lililofyatuliwa na helikopta ya Marekani katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Baghdad mji mkuu wa Iraq.
-
Joe Biden amkosoa vikali Trump kwa kutoa amri ya kuuliwa Jenerali Soleimani
Jan 03, 2020 08:35Joe Biden ambaye ni miongoni ma wanasiasa wa chama cha Democratic wanaochuana kupata tiketi ya kuwakilisha chama hicho katika uchaguzi ujao wa rais utakaofanyika mwaka huu nchini Marekani amemkosoa vikali Rais Donald Trump kwa kutoa amri ya kuuliwa shahidi Kamanda wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu nchini Iran, Meja Jenerali Qassem Soleimani.
-
Msemaji wa jeshi la SEPAH: Furaha ya Marekani na Israel itageuka kuwa maombolezo
Jan 03, 2020 08:21Msemaji wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu SEPAH, huku akiomboleza kuuawa shahidi Meja Jenerali Qassim Soleimani, Kamanda wa kikosi cha Quds cha jeshi hilo amesisitiza kwamba furaha ya muda mfupi ya Wamarekani na Wazayuni itageuka kuwa maombolezo hivi karibuni.
-
Mkuu wa Mahakama za Iran na Spika wa Bunge: Iran italipiza kisasi cha damu ya Jenerali Soleimani
Jan 03, 2020 08:10Mkuu wa Idara ya Vyombo vya Mahakama nchini Iran na Spika wa Majlisi ya Ushari ya Kiislamu (Bunge) hapa nchini wamesisitiza kuwa Jamhuri ya Kiislamu italipiza kisasi cha damu ya Shahidi Qassem Soleimani aliyeuawa mapema leo katika shambulizi la Marekani kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Baghdad nchini Iraq.
-
Muhammad Zarif: Kuuawa shahidi Soleimani kutaimarisha zaidi mapambano ya Kiislamu kieneo na kimataifa
Jan 03, 2020 08:04Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa kuuawa shahidi Meja Jenerali Qassim Soleimani, Kamanda wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Ulinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu katika shambulio la kigaidi lililotekelezwa na Marekani mapema leo Ijumaa, kutaimarisha zaidi mti wa mapambano ya Kiislamu katika eneo na ulimwengu mzima kwa ujumla.