-
Watu wa Afrika walaani jinai za utawala wa Israel dhidi ya Yemen na Gaza
Sep 05, 2025 06:54Wananchi wa nchi kadhaa za Afrika wamefanya maandamano makubwa kulaani jinai za utawala wa Kizayuni dhidi ya watu wa Yemen na Gaza, wakionesha mshikamano wa wazi na harakati za ukombozi wa Wapalestina.
-
DRC yapinga kupelekwa balozi mdogo wa Kenya mjini Goma
Aug 17, 2025 08:07Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo imepinga hatua ya Kenya ya kumteua balozi mdogo anayetazamiwa kutumwa katika mji wa Goma ulioko mashariki mwa DRC, ikiuelezea uamuzi huo kuwa "usiofaa".
-
IPOA yafichua: Polisi wa Kenya waliua watu 65 katika maandamano Juni, Julai
Jul 25, 2025 02:14Ripoti mpya ya Mamlaka Huru ya Kuchunguza Utendakazi wa Polisi (IPOA) imefichua kwamba watu 65 walipoteza maisha, 41 kati yao kwa kupigwa risasi na maafisa wa polisi, huku raia 342 wakijeruhiwa vibaya wakati wa maandamano ya Juni 25 na Julai 7 mwaka huu dhidi ya serikali ya Rais William Ruto wa Kenya.
-
Kaunti za Busia, Bungoma na Kakamega nchini Kenya zathibitisha maambukizo ya ugonjwa wa Mpox
Jul 23, 2025 08:37Magharibi mwa Kenya sasa ndio kitovu cha mlipuko wa ugonjwa wa Mpox huku kaunti za Busia, Bungoma na Kakamega nchini humo zikithibitisha kuwa na wagonjwa kadhaa walioambukizwa ugonjwa huo unaosababishwa na virusi.
-
Mwanaharakati wa haki za binadamu Kenya aachiwa kwa dhamana, ashtakiwa kwa kumiliki silaha kinyume cha sheria
Jul 21, 2025 10:08Boniface Mwangi, mwanaharakati wa haki za binadamu wa Kenya ambaye amekuwa na nafasi kuu katika maandamano dhidi ya serikali, ameachiwa huru kwa dhamana leo Jumatatu baada ya kushtakiwa kwa kupatikana na gesi ya kutoa machozi na silaha nyumbani kwake.
-
Umri wa unywaji pombe Kenya wapendekezwa kuongezwa kutoka miaka 18 hadi 21
Jul 17, 2025 08:07Mamlaka ya Taifa ya Kupambana na Matumizi ya Pombe na Dawa za Kulevya nchini Kenya (NACADA) imetetea pendekezo lake la kutaka umri wa kisheria wa kunywa pombe nchini humo uongezwe kutoka miaka 18 hadi 21, ikitaja utafiti wa kiafya, maoni ya umma na viwango vya kimataifa kama msingi wa pendekezo hilo.
-
Kadhaa wauawa katika shambulio la al-Shabaab, Garissa Kenya
Jul 14, 2025 11:42Watu wawili wameuawa huku wengine kadhaa wakijeruhiwa katika shambulio linaloshukiwa kuwa la magaidi wa al-Shabaab katika Kaunti ya Garissa, kaskazini mashariki mwa Kenya.
-
Baadhi ya Waislamu Kenya wapendekeza Kadhi Mkuu ajaye atoke nje ya Pwani
Jul 14, 2025 03:26Baada ya kupita siku chache tu tangu alipoaga dunia Kadhi Mkuu wa Kenye Sheikh Abdulhalim Hussein Athman, baadhi ya Waislamu wamependekeza kadhi ajaye atoke nje ya eneo la Pwani.
-
Mkuu wa Mawaziri Kenya atofautiana na Rais Ruto kuhusu kuwapiga risasi waandamanaji
Jul 13, 2025 23:43Mkuu wa Mawaziri wa Mawaziri nchini Kenya, Musalia Mudavadi ametofautiana na Rais William Ruto kuhusu wito wake wa kupigwa risasi viijana wanaoandamana kupinga sera za serikali yake na amevitaka vyombo vya usalama visiwaumize Wakenya wakati wa maandamano.
-
Kadhi Mkuu wa Kenya Sheikh Abdulhalim aaga dunia, amezikwa leo
Jul 10, 2025 09:43Kadhi Mkuu wa Kenya Sheikh Abdulhalim Hussein Athman amefariki dunia usiku wa manane wa kuamkia leo mjini Mombasa na maziko yake yamefanyika leo.