-
Kiongozi Muadhamu: Kuhitimishwa satwa ya Daesh ni pigo kwa Marekani na tawala tegemezi kwa Washington
Nov 22, 2017 04:37Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesisitiza kuwa, kuhitimishwa satwa ya mti khabithi wa kundi la kigaidi la Daesh ni pigo kwa serikali za huko nyuma na za sasa za Marekani pamoja na tawala vibaraka na tegemezi kwa Washington katika Mashariki ya Kati ambazo zililianzisha kundi hili na kuliunga mkono kwa hali na mali ili zitanue satwa zao katika eneo hili na hivyo kuufanya utawala ghasibu wa Israel uwe na udhibiti wa eneo hili.
-
Ujumbe wa Jenerali Suleimani kwa Kiongozi Muadhamu, satwa ya ISIS imeangamizwa
Nov 21, 2017 04:28Kamanda wa Kikosi cha Quds katika Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu, IRGC, amemtumia ujumbe Ayatullah Sayyed Ali Khamenei Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu akitangaza kuangamizwa satwa khabithi ya kundi la kigaidi la ISIS au Daesh.
-
Kiongozi Muadhamu akagua maeneo yaliyoathiriwa na tetemeko la ardhi katika mkoa wa Kermanshah
Nov 20, 2017 04:46Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Sayyid Ali Khamenei mapema leo ameelekea mkoani Kermanshah katika safari ya ghafla ya kukagua maeneo yaliyokumbwa na tetemeko la ardhi pamoja na kuonana na wananchi walioathirwa na janga hilo la kimaumbile.
-
Kiongozi Muadhamu atoa wito kwa viongozi kufanya hima ya kuwafikishia misaada waathirika wa tetemeko la ardhi
Nov 13, 2017 04:54Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ametoa ujumbe maalumu kufuatia tetemeko la ardhi lililotokea magharibi mwa Iran na kusababisha vifo vya mamia ya watu na wengine wengi kujerihiwa
-
Kiongozi Muadhamu: Masafa yaliyokatwa na Mapinduzi ya Kiislamu yanaleta matumaini mengi
Nov 09, 2017 13:51Husainia ya Imam Khomeini MA hapa mjini Tehran leo ilikuwa mwenyeji wa ujumbe mbalimbali wa wanachuo kutoka kona zote za Iran ikiwa ni sehemu ya kumbukumbu za Arubaini ya Bwana wa Mashahidi, Aba Abdillahil Husain AS na wafuasi wake waaminifu, ambapo wanafunzi hao wa vyuo vikuu walikwenda kumtembelea Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kama sehemu ya maadhimisho hayo.
-
Kiongozi Muadhamu: Matembezi ya Arubaini ya Imam Hussein AS ni nembo ya hali ya juu
Nov 07, 2017 10:51Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amezungumzia matembezi ya Arubiani ya Imam Hussein AS na kusema: "Wamebahatika wale ambao wako katika matembezi ya kuelekea katika Ziara ya Arubaini ambao wataisoma Ziara hiyo Siku ya Arubaini wakimhutubu Imam Hussein AS, Imamu wa tatu wa Mashia duniani."
-
Kiongozi: Hatua zichukuliwe dhidi ya wanaovuruga uhusiano wa Iran na Jamhuri ya Azerbaijan
Nov 02, 2017 01:15Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesisitiza kuwa kuna wanaopinga uhusiano wa karibu na wa udugu baina ya Iran na Jamhuri ya Azerbaijan, na kwa msingi huo kuna ulazima wa kukabiliana na wanaotekeleza njama hizo.
-
Kiongozi Muadhamu: Nguvu za kiulinzi za Iran si kitu cha kujadiliwa kabisa
Oct 25, 2017 13:14Amirijeshi Mkuu wa vikosi vyote vya ulinzi vya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, uwezo na nguvu za kiulinzi za Iran si kitu cha kujadiliwa kabisa kama ambavyo zana zozote za ulinzi na kitu chochote kile kinacholeta nguvu za taifa la Iran si kitu cha kufanyiwa muamala wa aina yoyote ile.
-
Kiongozi Muadhamu: Kama upande wa pili utayachana makubaliano ya JCPOA, Iran itayararua vipande vipande
Oct 18, 2017 11:51Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesisitiza kuwa, Iran haitayachana makubaliano ya nyuklia ya JCPOA maadamu upande wa pili haujayachana, lakini kama upande huo utayachana, basi Jamhuri ya Kiislamu ya Iran itayararua vipande vipande makubaliano hayo.
-
Kiongozi Muadhamu: Utawala wa Kizayuni unataka kuunda Israel mpya katika eneo hili
Oct 04, 2017 14:39Ayatullah Sayyid Ali Khamenei, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu leo usiku ameonana na Rais Recep Tayyip Erdogan na ujumbe alioandamana nao hapa mjini Tehran na kusisitiza kwamba kuna ulazima wa kuongezwa kiwango cha ushirikiano wa nchi mbili kama ambavyo pia ni jambo muhimu sana kuweko maelewano na ushirikiano baina ya Iran na Uturuki katika masuala muhimu ya ulimwengu wa Kiislamu.