-
Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu: Hija ni fursa bora ya kuzima harakati za kipropaganda za maadui
Oct 03, 2017 12:33Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema kuna kambi kubwa ya kimataifa ya propaganda dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na kusisitiza kwamba: fursa ya Hija ni minbari bora kabisa ya tablighi kwa ajili ya kujenga mawasiliano na walimwengu na kuzima propaganda za upande wa pili.
-
Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu: Maadui wanafanya njama za kuzuia jihadi ya taifa la Iran
Oct 03, 2017 12:31Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amezungumzia jitihada kubwa zinazofanywa na maadui kwa ajili ya kuliondoa taifa la Iran hususan vijana katika njia ya jihadi na kufa shahidi, kulifanya limsahau Imam Khomeini na kupotea njia ya wazi ya Mapinduzi ya Kiislamu na kusema kuwa: Kuvutiwa kwa nyoyo za vijana wengi kwenye masuala ya kimapinduzi katika mazingira kama haya ni jambo la kustaajabisha.
-
Kiongozi Muadhamu: Mwenyezi Mungu amemfanya shahidi Hojaji kuwa kipenzi cha watu
Sep 27, 2017 10:33Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesisitiza kuwa, ikhlasi, nia safi na kufanya harakati kwa wakati na kuhitajia jamii kuuawa shahidi kama huku ni mambo ambayo yamepelekea Mwenyezi Mungu amfanye shahidi Mohsen Hojaji kuwa kipenzi cha watu wote.
-
Kiongozi Muadhamu ashiriki katika kuuaga mwili wa shahid Hojaji
Sep 27, 2017 06:30Ayatullah Sayyid Ali Khamenei, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, alfajiri ya leo Jumatano amekwenda katika Msikiti wa Imam Husain AS hapa Tehran na kuusomea Faatiha mwili mtoharifu wa shahid Mohsen Hojaji, aliyeuliwa shahidi na magaidi wa Daesh wakati akilinda Haram ya mjukuu wa Bwana Mtume Muhammad SAW, Bibi Zaynab al Kubra AS nchini Syria.
-
Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu: Wamarekani wanapaswa kuona aibu kwa kuwa na Rais kama Trump
Sep 21, 2017 11:46Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Ali Khamenei amekosoa vikali matamshi ya kipumbavu, kijinga na yaliyojaa urongo yaliyotolewa na Rais wa Marekani katika mkutano wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa mjini New York na kusema kuwa: Matamshi hayo hayakutokana na nguvu bali yametokana na ghadhabu, kuchanganyikiwa na akili finyu.
-
Kiongozi Muadhamu: Ufumbuzi wa suala la Myanmar ni nchi za Kiislamu kuchukua hatua za kivitendo
Sep 12, 2017 03:26Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amekosoa kimya na kutochukua hatua jumuiya za kimataifa na wanaojigamba kuwa watetezi wa haki za binadamu kuhusiana na matukio ya maafa yanayojiri Myanmar na kusisitiza kwamba: Njia ya utatuzi wa kadhia hii ni kuchukuliwa hatua za kivitendo na nchi za Kiislamu na kuishinikiza kisiasa na kiuchumi serikali isiyo na huruma ya Myanmar.
-
Kiongozi Muadhamu: Kulindwa moyo wa kimapinduzi na kidini katika udiplomasia ni jambo la dharura
Aug 26, 2017 11:22Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu leo Jumamosi ameonana na Rais Rouhani na baraza lake la mawaziri na kusema kuwa, kulindwa msimamo na muelekeo wa kimapinduzi na kidini katika siasa za kigeni za Iran ni jambo muhimu sana.
-
Ayatullah Shahroudi ateuliwa Mkuu wa Halmashauri ya Kuainisha Maslahi ya Mfumo wa Jamhuri ya Kiislamu
Aug 14, 2017 10:52Ayatullah Sayyid Ali Khamenei, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amemteua Ayatullah Sayyid Mahmoud Hashemi Shahroudi kuwa Mwenyekiti wa Halmashauri ya Kuainisha Maslahi ya Mfumo wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kwa muhula wa miaka mitano.
-
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi aidhinisha kura za wananchi na kumpasisha Rouhani kuwa Rais wa Iran
Aug 03, 2017 03:51Sherehe ya kuidhinisha kura za wananchi kwa Rais wa Jamhuri ya Kiislamu zimefanyika leo asubuhi katika Husseiniya ya Imamu Khomeini (M.A) hapa Tehran kwa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kumpasisha Hassan Rouhani kuwa Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.
-
Kiongozi Muadhamu alishukuru jeshi la SEPAH, kwa kushambulia maeneo ya magaidi Syria
Jul 05, 2017 23:40Saa moja baada ya Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran SEPAH kushambulia kwa makombora maeneo ya magaidi wa kundi la Daesh huko Deir Ezzor nchini Syria, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, alikutana na makamanda wa SEPAH na kuwashukuru kutokana na hatua yao hiyo.