Kiongozi Muadhamu: Mwenyezi Mungu amemfanya shahidi Hojaji kuwa kipenzi cha watu
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i34919-kiongozi_muadhamu_mwenyezi_mungu_amemfanya_shahidi_hojaji_kuwa_kipenzi_cha_watu
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesisitiza kuwa, ikhlasi, nia safi na kufanya harakati kwa wakati na kuhitajia jamii kuuawa shahidi kama huku ni mambo ambayo yamepelekea Mwenyezi Mungu amfanye shahidi Mohsen Hojaji kuwa kipenzi cha watu wote.
(last modified 2026-02-22T02:21:18+00:00 )
Sep 27, 2017 14:03 UTC
  • Kiongozi Muadhamu: Mwenyezi Mungu amemfanya shahidi Hojaji kuwa kipenzi cha watu

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesisitiza kuwa, ikhlasi, nia safi na kufanya harakati kwa wakati na kuhitajia jamii kuuawa shahidi kama huku ni mambo ambayo yamepelekea Mwenyezi Mungu amfanye shahidi Mohsen Hojaji kuwa kipenzi cha watu wote.

Ayatullah Sayyid Ali Khamenei amesema hayo leo katika msikiti wa Imam Hussein as mjini Tehran kando ya mwili wa shahidi mlinzi wa haram Mohsen Hojaji  na kuongeza kuwa, mashahidi wote ni azizi na vipenzi mbele ya Mwenyezi Mungu, lakini kuna sifa maalumu kwa kijana huyu ambayo imepelekea Mwenyezi Mungu alinyanyue juu jina lake.

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amebainisha kwamba, tazameni kutokana na kuuawa shahidi Mohsen Hojaji ni kwa jinsi gani kunashuhudiwa hekaheka katika kila kona ya Iran za kumuadhimisha na kumuaga shahidi huyu.

Ayatullah Khamenei amemsifu shahid Hojaji kwa kujitolea kwake katika njia ya Mwenyezi Mungu na kumuomba Allah ampandishe daraja za juu za utukufu kama ambavyo pia amemuomba Mwenyezi Mungu azidishe subira na uvumilivu katika nyoyo za watu wa familia yake.

Umati wa watu walioshiriki katika shughuli ya kuuaga mwili wa shahidi Mohsen Hojaji

Shughuli ya kuuaga na kuusindikiza mwili wa shahidi Mohsen Hojaji imefanyika leo hapa Tehran na baadaye mwili wake utapelekwa kijijini kwao katika mkoa wa Isfahan wa katikati mwa Iran kwa ajili ya maziko hiyo kesho Alkhamisi.

Ikumbukwe kuwa, tarehe 9 Agosti 2017, kundi la kigaidi la Daesh lilimuua shahidi kijana huyo muumini ambaye kwa mapenzi yake makubwa kwa watu wa nyumba tukufu ya Bwana Mtume Muhammad SAW alikwenda nchini Syria kulinda haram za watukufu hao dhidi ya hujuma za magenge ya kigaidi kama vile Daesh.