Kiongozi Muadhamu alishukuru jeshi la SEPAH, kwa kushambulia maeneo ya magaidi Syria
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i31392-kiongozi_muadhamu_alishukuru_jeshi_la_sepah_kwa_kushambulia_maeneo_ya_magaidi_syria
Saa moja baada ya Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran SEPAH kushambulia kwa makombora maeneo ya magaidi wa kundi la Daesh huko Deir Ezzor nchini Syria, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, alikutana na makamanda wa SEPAH na kuwashukuru kutokana na hatua yao hiyo.
(last modified 2023-11-27T12:14:11+00:00 )
Jul 06, 2017 04:10 UTC
  • Kiongozi Muadhamu alishukuru jeshi la SEPAH, kwa kushambulia maeneo ya magaidi Syria

Saa moja baada ya Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran SEPAH kushambulia kwa makombora maeneo ya magaidi wa kundi la Daesh huko Deir Ezzor nchini Syria, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, alikutana na makamanda wa SEPAH na kuwashukuru kutokana na hatua yao hiyo.

Taarifa iliyoandiwa na ofisi ya kutunza na kusambaza athari za Ayatullah Ali Khamenei, imesema kuwa, katika kikao hicho, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu alilitaja shambulio la makombora katika ngome za magaidi nchini Syria kuwa ni kitendo kitukufu na kumwomba Mwenyezi Mungu aipokee ibada ya Mwezi wa Ramadhani ya Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran SEPAH.

Moja ya makombora hayo 

Kiongozi Muadhamu ambaye ni amiri jeshi mkuu wa vikosi vyote nchini Iran amebainisha kuwa, maadui wanafuatilia sana suala la makombora ya taifa hili na kulitaka jeshi la Iran kufanya juhudi kubwa katika uga wa makombora ili maadui wakate tamaa. Aidha katika kikao hicho Ayatullah Sayyid Ali Khemeni, sambamba na kupitia ripoti ya mafanikio ya operesheni ya makombora dhidi ya ngome za wanachama wa kundi la kigaidi na ukufurishaji la Daesh amesisitiza kuwa, operesheni hiyo iliyofanyika kwa kuongozwa na intelejensia ya Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran SEPAH, ililenga tu maeneo ya magaidi na hakuna raia hata mmoja ambaye aliguswa na shambulizi hilo.

Magaidi wa Daesh wakiwa wameangamizwa

Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran SEPAH lilishambulia maeneo ya magaidi huko Deir Ezzor nchini Syria tarehe 18 Juni mwaka huu, ambapo zaidi ya magaidi 170 wakiwamo makamanda wa ngazi ya juu wa genge la Daesh waliangamizwa sambaba na kuharibiwa kabisa ngome zao hizo.