Kiongozi Muadhamu: Masafa yaliyokatwa na Mapinduzi ya Kiislamu yanaleta matumaini mengi
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i36282-kiongozi_muadhamu_masafa_yaliyokatwa_na_mapinduzi_ya_kiislamu_yanaleta_matumaini_mengi
Husainia ya Imam Khomeini MA hapa mjini Tehran leo ilikuwa mwenyeji wa ujumbe mbalimbali wa wanachuo kutoka kona zote za Iran ikiwa ni sehemu ya kumbukumbu za Arubaini ya Bwana wa Mashahidi, Aba Abdillahil Husain AS na wafuasi wake waaminifu, ambapo wanafunzi hao wa vyuo vikuu walikwenda kumtembelea Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kama sehemu ya maadhimisho hayo.
(last modified 2026-01-14T11:42:18+00:00 )
Nov 09, 2017 17:21 UTC
  • Kiongozi Muadhamu: Masafa yaliyokatwa na Mapinduzi ya Kiislamu yanaleta matumaini mengi

Husainia ya Imam Khomeini MA hapa mjini Tehran leo ilikuwa mwenyeji wa ujumbe mbalimbali wa wanachuo kutoka kona zote za Iran ikiwa ni sehemu ya kumbukumbu za Arubaini ya Bwana wa Mashahidi, Aba Abdillahil Husain AS na wafuasi wake waaminifu, ambapo wanafunzi hao wa vyuo vikuu walikwenda kumtembelea Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kama sehemu ya maadhimisho hayo.

Kwa upande wake, Ayatullah Sayyid Ali Khamenei, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ametoa hotuba fupi mbele ya wanachuo hao na sambamba na kuzitukuza kumbukumbu zilizofana za Arubaini ya Imam Husain AS amesema kuwa, mikusanyiko ya namna hii inabidi itie nguvu na kumarisha nia na azma za watu wote na ni muhimu kuwa imara katika njia hiyo na kutotetereshwa na misukosuko na matatizo mbalimbali yanayotokea.

Ayatullah Sayyid Ali Khamenei, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislalmu

Ayatullah Khamenei ameongeza kuwa, kufanya jihadi katika njia ya Allah, kusimamisha haki na uadilifu na kufikia kwenye ustaarabu na jamii ya Kiislamu ni njia nzito yenye misukosuko na pandashuka nyingi, lakini mtu anapoangalia masafa ambayo Mapinduzi ya Kiislamu yameshayavuuka hadi hivi sasa na anapoangalia upeo ulioko mbele, anaona dalili za wazi za kufanikiwa kikamlifu katika jitihada hizo.

Mwishoni mwa maadhimisho hayo, Ayatullah Sayyid Ali Khamenei amewasalisha hadhirina sala za Adhuhuri na Alaasiri.