-
Kiongozi wa Mapinduzi: Mwaka 1404 ni "Mwaka wa Uwekezaji kwa ajili ya Uzalishaji"
Mar 20, 2025 07:42Ayatullah Khamenei Kiongozi Muadhamu uwa Mapinduzi ya Kiislamu ametuma ujumbe kwa mnasaba wa kuanza mwaka mpya wa 1404 hijria shamsia na kuutaja mwaka huu mpya kuwa ni "Mwaka wa Uwekezaji kwa ajili ya Uzalishaji."
-
Kiongozi Muadhamu: Iran inakabiliwa na muungano wa madola ya kinafiki
Mar 03, 2025 03:38Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatullah Sayyid Ali Khamenei amesema Jamhuri ya Kiislamu haina tatizo na mataifa mengine; lakini hata hivyo inakabiliwa na muungano mpana wa "madola ya kinafiki" yanayojaribu kuingilia mambo yake ya ndani na kuvuruga uhusiano wake wa nje.
-
Mwakilishi wa Kiongozi wa Mapinduzi awasalia Mashahidi wa Hizbullah, bahari ya umati wa watu yaifunika Beirut
Feb 23, 2025 11:28Sheikh Muhammad Yazbek, Mwakilishi wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ameongoza Sala ya Maiti ya kusalia miili ya Mashahidi Sayyid Hassan Nasrullah na Sayyid Hashim Safiyyuddin katika mazishi ya kihistoria yaliyofanyika leo katika mji mkuu wa Lebanon, Beirut.
-
Kiongozi Muadhamu: Maandamano dhidi ya Israel yanaashiria kuungwa mkono zaidi Palestina duniani
Feb 22, 2025 08:36Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatullah Sayyid Ali Khamenei amesema maandamano na mikusanyiko dhidi ya Israel barani Ulaya na Marekani inaashiria kuongezeka mshikamano wa kimataifa na taifa la Palestina.
-
Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu: Mpango wa kijinga wa Marekani kuhusu Gaza hautafika popote
Feb 18, 2025 11:45Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu, akiwapongeza wapiganaji wa Muqawama kwa ushindi wao katika Ukanda wa Gaza, amesisitiza kwamba kazi kubwa ya viongozi na wapiganaji wa Muqawama wa Palestina ipo katika "umoja na mshikamano" na "kusimama imara" dhidi ya adui, kuendesha mchakato mgumu wa mazungumzo, pamoja na uvumilivu na ustahimilivu wa wananchi, ambavyo vimeinua heshima ya Muqawama katika eneo.
-
Imam Khamenei: Wairani wamepuuza vitisho vya kijinga vya adui na kutuma ‘ujumbe wa umoja’ kwenye maadhimisho ya Bahman 22
Feb 12, 2025 10:37Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatullah Sayyid Ali Khamenei amelipongeza taifa la Iran kwa kufikisha "ujumbe wa umoja" kwa jamii ya kimataifa katika maadhimisho ya miaka 46 ya Ushindi wa Mapinduzi ya Kihistoria ya Kiislamu ya Iran ya mwaka 1979.
-
Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu: Kufanya mazungumzo na Marekani si jambo la werevu, mantiki, wala heshima
Feb 07, 2025 07:17Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema katika mkutano na makamanda na wafanyakazi wa Kikosi cha Anga na cha Ulinzi wa Anga vya Jeshi la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kwamba kufanya mazungumzo na Marekani si jambo la werevu, mantiki, wala heshima.
-
Kiongozi Muadhamu awasamehe wafungwa zaidi ya 3,000 kwa mnasaba wa maadhimisho ya Mapinduzi ya Kiislamu
Feb 05, 2025 11:25Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatullah Sayyid Ali Khamenei, ameidhinisha kusamehewa kikamilifu au sehemu ya adhabu wafungwa zaidi ya 3,000 katika maadhimisho ya mwaka wa 46 wa Mapinduzi ya Kiislamu.
-
Kiongozi Muadhamu amteua Naim Qassem kuwa mwakilishi wake Lebanon
Feb 05, 2025 08:59Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Sayyid Ali Khamenei, katika dikrii, amemuarifisha Katibu Mkuu wa Harakati ya Muqawamaya ya Hizbullah, Sheikh Naim Qassem kama mwakilishi wake nchini Lebanon.
-
Imam Khamenei: Gaza imezipiga mweleka Marekani na Israel kwa Neema za Allah
Feb 02, 2025 09:35Kiongozi Muadhami wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatullah Sayyid Ali Khamenei amesema hakuna mtu yeyote angelifikiria mwaka jana kwamba, Wapalestina wa Ukanda wa Gaza wangeliibuka washindi dhidi ya muungano wa Marekani na Israel.