Jul 29, 2020 07:25
Leo ni siku ya pili na ya mwisho ya mazoezi makubwa ya kijeshi ya pamoja yaliyopewa jina la Mtumu Mtukufu (SAW) 14. Mazoezi hayo ni ya pamoja ya vikosi vya majini na vya anga vya Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu na yanafanyika katika eneo la Hormozgan, magharibi mwa Lango Bahari la Hormoz, Ghuba ya Uajemi na maeneo mengine ya nchi.