-
Mangoush: Libya haitaruhusu ardhi yake itumiwe dhidi ya nchi nyingine
Jun 11, 2021 22:21Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa nchini Libya amesema kuwa nchi yake haitakubali kutumiwa kama kituo cha kuvuruga amani na utulivu katika kanda hiyo ya Afrika au kutumiwa ardhi na anga yake dhidi ya upande wowote mwingine.
-
Hatua mpya za vikwazo vya Marekani dhidi ya Iran
Jun 11, 2021 08:25Wizara ya Biashara ya Marekani Alkhamisi ya jana iliwaweka watu na mashirika kadhaa katika orodha yake ya vikwazo kwa kisingizio cha nafasi yao katika kudhamini fedha kwa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (Sepah) na harakati ya wapiganaji wa kujitolea ya Ansarullah nchini Yemen.
-
Russia yaanza mazoezi ya kijeshi eneo ambako Marekani pia inapanga mazoezi ya kivita
Jun 11, 2021 07:53Jeshi la Majini la Russia limeanza mazoezi makubwa ya kijeshi katika eneo la kati mwa Bahari ya Pasifiki punde baada ya Marekani kusema itafanya mazoezi makubwa zaidi ya kivita katika eneo hilo hilo katika msimu wa joto mwaka huu.
-
Ansarullah: Marekani inafadhilisha vita Yemen, haitaki amani
Jun 11, 2021 03:25Mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Mapinduzi ya Yemen amelaani hatua ya Marekani ya kuliwekea vikwazo vipya taifa hilo la Kiarabu na kusisitiza kuwa, Washington inafadhilisha vita nchini Yemen, na wala haitaki amani kama inavyodai.
-
Pentagon yaingiwa na kiwewe baada ya manowari za Iran kuwasili Atlantic
Jun 10, 2021 22:22Wizara ya Ulinzi ya Marekani (Pentagon) imeingiwa na kiwewe na wahaka mkubwa baada ya msafara wa meli za kijeshi za Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kuwasili katika Bahari ya Atlantic pasi na kupitia katika bandari za nchi nyingine kwa mara ya kwanza katika historia.
-
Russia: Wanajeshi wa Marekani nchini Syria ni wavamizi, waondoke
Jun 09, 2021 07:08Waziri wa Mambo ya Nje wa Russia amesema kuwa, wanajeshi wa Marekani ni wavamizi nchini Syria na wako huko kinyume cha sheria, hivyo wanapaswa waondoke.
-
Eritrea yailaumu Marekani kwa kuchochea mapigano Tigray, Ethiopia
Jun 08, 2021 03:42Waziri wa Mambo ya Nje wa Eritrea amezilaumu tawala za Marekani kwa kuchochea mapigano na vita katika eneo la Tigray, la kaskazini mwa Ethiopia kwa zaidi ya miongo miwili sasa.
-
Vikwazo vya Marekani kipindi cha corona ni ukiukaji wa haki za binadamu
Jun 05, 2021 22:07Wimbi la maambukizi ya virusi vya corona linaendelea kuchukua roho za watu katika nchi mbalimbali duniani huku jumuiya za kimataifa zikisisitiza udharura wa kutolewa chanjo ya kukabiliana na virusi hivyo na kusambazwa chanjo hiyo na vifaa vingine vya tiba ili kufanikisha jitihada za kuvuka kipindi cha sasa cha janga hilo la kimataifa.
-
Upinzani Bahrain wailaani US kupeperusha 'bendera ya ushoga' Manama
Jun 05, 2021 21:56Chama kimoja cha upinzani nchini Bahrain kimekosoa vikali hatua ya Marekani ya kupeperusha bendera yenye nembo ya kuunga mkono ushoga katika ubalozi wake mjini Manama.
-
Viongozi wa Marekani waendelea na madai yao ya kuijenga upya Ghaza
Jun 05, 2021 07:21Mwakilishi wa kudumu wa Marekani katika Umoja wa Mataifa ameendeleza madai ya viongozi wa nchi hiyo kuhusu kuujenga upya Ukanda wa Ghaza. Amedai kuwa Washington inafanya juhudi za kukusanya misaada ya kimataifa ya kuujenga upya ukanda huo.