Guterres azitaka Marekani na Russia kudhibiti silaha zao za nyuklia
https://parstoday.ir/sw/news/world-i73358-guterres_azitaka_marekani_na_russia_kudhibiti_silaha_zao_za_nyuklia
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ametoa wito kwa Marekani na Russia akizitaka kudhibiti silaha za nyuklia.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Aug 10, 2021 05:21 UTC
  • Antonio Guterres
    Antonio Guterres

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ametoa wito kwa Marekani na Russia akizitaka kudhibiti silaha za nyuklia.

Antonio Guterres amezitaka nchi zote wanachama katika Mkataba wa Kuzuia Silaha za Nyuklia (NPT) kuchukua hatua za kufuta kabisa uwezekano wa kutumia silaha za nyuklia.

Wito huo wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa umetolewa siku kadhaa baada ya Guterres mwenyewe kueleza wasiwasi wake kutokana na kutokuwepo maendeleo katika juhudi za kuangamia kabisa silaha za nyuklia duniani na kuzitaka nchi zinazomiliki silaha hizo kuziangamiza. 

Nchi 191 duniani, ikiwemo Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, ni wanachama wa Mkataba wa Kuzuia Silaha za Nyuklia (NPT). Utawala haramu wa Israel umekata kujiunga na mkataba huo. 

 Canada, Israel, Marshall, Micronesia, Palau Marekani zimekataa kutia saini mkataba huo. 

Utawala wa Kizayuni wa Israel ambao umejilimbikizia silaha kadhaa za nyuklia unahatarisha eneo la Magharibi mwa Asia na dunia nzima kwa ujumla. Utawala huo pia umekataa kujiunga na Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Nyuklia (IAEA).