-
Malengo halisi ya Magharibi kuhusu Iran ni yapi?
Jul 30, 2025 08:29Vyombo vya habari vya kigeni, sambamba na kuripoti kauli ya hivi karibuni ya Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu, vimezingatia kwa namna ya kipekee sehemu ya hotuba yake ambapo amesisitiza kuwa: “Mpango wa nyuklia, urutubishaji na haki za binadamu ni visingizio – wanachotaka wao ni dini na elimu yenu.”
-
Imam Khamenei: Suala la nyuklia na haki za binadamu ni visingizio tu, Marekani haifurahishwi na uwezo wa Jamhuri ya Kiislamu
Jul 29, 2025 23:53Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema, sababu kuu ya upinzani wa ubeberu wa dunia unaoongozwa na Marekani mtenda jinai dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ni dini, elimu na umoja wa Wairani chini ya kivuli cha Qur'ani Tukufu na Uislamu.
-
Kwa nini Marekani imeitaka China iache kununua mafuta ya Iran?
Jul 27, 2025 23:03Waziri wa Fedha wa Marekani ametoa wito kwa China kuacha kununua mafuta ya Iran na Russia wakati huu inapokaribia duru mpya ya mazungumzo ya ushuru wa forodha kati ya Marekani na China.
-
Helikopta ya Jeshi la Wanamaji la Iran yaitimua manowari ya US katika Bahari ya Oman
Jul 24, 2025 03:25Helikopta ya Jeshi la Wanamaji la Iran imeitimua manowari ya mashambulizi ya Marekani iitwayo USS Fitzgerald katika Bahari ya Oman, kwa kutoa ishara za onyo na hatimaye kuilazimisha ibadili mkondo wake kuelekea upande wa kusini wa eneo hilo.
-
Kwa nini Marekani imejiondoa rasmi UNESCO?
Jul 23, 2025 05:28Marekani ilitangaza Jumanne, Julai 22, kwamba imejiondoa rasmi katika Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni UNESCO.
-
Uingereza yadokeza kuwa itachukua hatua zaidi dhidi ya Israel kutokana na hali ya 'kikatili' ya Ghaza
Jul 23, 2025 02:41Waziri wa mambo ya nje wa Uingereza David Lammy ameonya kuwa ikiwa usitishaji vita katika Ukanda wa Ghaza hautafikiwa hivi karibuni, zinaweza kuchukuliwa hatua zaidi dhidi ya Israel.
-
Mafaili ya siri yanayohusu mauaji ya Martin Luther King Jr yawekwa hadharani
Jul 23, 2025 00:18Serikali ya Rais wa Marekani Donald Trump imeweka hadharani maelfu ya mafaili na nyaraka za serikali zinazohusiana na mauaji ya nyota wa kupigania haki za kiraia Martin Luther King Jr. Siku ya Jumatatu, kurasa zipatazo 240,000 ziliwekwa kwenye tovuti ya Hifadhi ya Taifa, ambayo imeahidi kutoa nyaraka nyingi zaidi.
-
Ripoti: Mienendo ya Netanyahu inaitia wasiwasi White House
Jul 20, 2025 10:50Baadhi ya maafisa wakuu wa Marekani wameliambia shirika la habari la Axios kwamba, hofu inaongezeka ndani ya utawala wa Donald Trump juu ya tabia na mienendo ya Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu, wakielezea mienendo hiyo kama ya kutojali, kuvuruga uthabiti, na wakati mwingine yenye ukosefu wa ukomavu.
-
Serikali ya Trump kuteketeza tani 500 za chakula, dunia ikisakamwa na njaa
Jul 18, 2025 13:40Marekani inajiandaa kuharibu karibu tani 500 za chakula cha msaada wa dharura, ikiwa ni sehemu ya hifadhi kubwa ya tani 60,000 za chakula hicho iliyokwama katika maghala katika sehemu mbalimbali duniani, huku njaa ikiongezeka kote ulimwenguni.
-
Afisa wa zamani wa Pentagon: Huenda US ikaishiwa na makombora
Jul 18, 2025 10:44Mshauri wa zamani wa Wizara ya Ulinzi ya Marekani (Pentagon), Douglas Macgregor ameonya kuwa, Marekani inaweza kuishiwa na hifadhi yake ya makombora ndani ya siku nane.