-
Los Angeles Times: Wakati umefika kwa majimbo ya Marekani kujitangazia uhuru wao
Apr 24, 2020 02:39Gazeti la Los Angeles Times la nchini Marekani limeandika kuwa, janga la corona nchini humo limeonesha kuwa wakati umefika kwa kila jimbo la Marekani kujitenga na kujitangazia uhuru wake.
-
Iran: Tuko tayari kuwasaidia wananchi wa Marekani wanaoteseka kwa corona
Apr 24, 2020 02:39Waziri wa Afya wa Iran amejibu maneno ya kijuba ya waziri wa afya wa Marekani aliyedai kuwa nchi yake iko tayari kuisaidia Iran kupambana na corona akisisitiza kuwa, Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imeonesha kivitendo uwezo wake mkubwa wa kakabiliana na matatizo kama haya ya corona na kuongeza kuwa, Tehran iko tayari kuwasaidia wananchi wa Marekani wanaoteseka kwa maradhi ya COVID-19 hivi sasa kutokana na uzembe wa serikali yao.
-
Iran yalaani chokochoko za Marekani Ghuba ya Uajemi, yamuita balozi wa Uswisi
Apr 23, 2020 22:15Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amekosoa vikali chokochoko za jeshi la Marekani dhidi ya wanajeshi wa baharini wa Iran katika Ghuba ya Uajemi, sambamba na kukosoa bwabwaja na vitisho vya Rais Donald Trump dhidi ya askari hao wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (SEPAH).
-
China yaipa WHO dola milioni 50 baada ya US kulikatia misaada shirika hilo la UN
Apr 23, 2020 22:02China imeliongeza Shirika la Afya Duniani (WHO) msaada wa dola milioni 30 za Marekani za kudhibiti mlipuko wa maambukizi ya virusi vya Corona duniani, siku chache baada ya Marekani kuikatia misaada taasisi hiyo ya Umoja wa Mataifa.
-
Meli 26 za kivita za Marekani zakumbwa na virusi vya Corona
Apr 23, 2020 03:05Afisa mmoja wa kijeshi nchini Marekani amesema kuwa meli 26 za kivita za nchi hiyo zimekumbwa na virusi vya Corona.
-
Mgogoro wa Venezuela: Serikali na wapinzani waanza mazungumzo ya siri
Apr 22, 2020 22:14Serikali ya Venezuela na wapinzani wa nchi hiyo wameanza duru mpya ya mazungumzo ya siri yenye lengo la kuupatia ufumbuzi mgogoro wa kisiasa wa nchi hiyo.
-
Trump akiri Marekani inatumia gharama kubwa isiyo na faida yoyote Asia Magharibi
Apr 22, 2020 22:13Baada ya mashambulizi ya Septemba 11, 2001 Marekani kwa kisingizio cha kupambana na ugaidi, ilielekeza majeshi yake katika eneo la Asia Magharibi.
-
Marekani yaelemewa na janga la Corona, yapewa msaada na Misri
Apr 22, 2020 08:23Misri imetuma nchini Marekani ndege iliyosheheni vifaa na zana za kitiba za kukabiliana na virusi vya Corona, wakati huu ambapo nchi hiyo inayotajwa kuwa dola kubwa na lenye uwezo zaidi duniani linaendelea kulemewa na janga ugonjwa wa Covid-19.
-
Rais Rouhani: Inapasa nchi zote zitangaze misimamo yao kuhusu hatua za kiuadui za Marekani
Apr 21, 2020 22:44Rais Hassan Rouhani amesema: Katika mazingira maalumu ya hivi sasa yanayotokana na kuenea virusi vya corona duniani, nchi zote zinapaswa kuwa bega kwa bega katika kupambana na kirusi hicho angamizi na kutangaza kwa uwazi kabisa misimamo yao kuhusiana na hatua za kiuadui za Marekani.
-
Marekani ndiyo ilipanga mashambulizi ya hivi karibuni ya Daesh nchini Iraq
Apr 21, 2020 07:17Mjumbe wa Kamisheni ya Usalama wa Taifa katika Bunge la Iraq amesema kuwa Wamarekani ndio waliopanga mashambulizi ya hivi karibuni ya magaidi wa kundi la kigaidi na ukufurishaji la Daesh (ISIS) nchini humo.