Marekani ndiyo ilipanga mashambulizi ya hivi karibuni ya Daesh nchini Iraq
(last modified Tue, 21 Apr 2020 11:47:29 GMT )
Apr 21, 2020 11:47 UTC
  • Marekani ndiyo ilipanga mashambulizi ya hivi karibuni ya Daesh nchini Iraq

Mjumbe wa Kamisheni ya Usalama wa Taifa katika Bunge la Iraq amesema kuwa Wamarekani ndio waliopanga mashambulizi ya hivi karibuni ya magaidi wa kundi la kigaidi na ukufurishaji la Daesh (ISIS) nchini humo.

Kirim Alivi, Mjumbe wa Kamisheni ya Usalama na Ulinzi katika Bunge la Iraq ameongeza kuwa, mashambulizi ya hivi karibuni ya genge la Daesh (ISIS) katika maeneo tofauti ya nchi hiyo, yalitekelezwa baada ya bunge la Iraq kupitisha uamuzi wa kutimuliwa askari vamizi wa Marekani katika ardhi ya Iraq. Alivi ameongeza kuwa, Wamarekani wana wasi wasi mkubwa kufuatia makundi ya kisiasa kufungamana na uamuzi wa kufukuzwa askari wa kigeni nchini Iraq na ni kwa ajili hiyo ndio maana wanaliunga mkono kundi la Daesh kwa lengo la kushadidisha mashinikizo kwa serikali ya Baghdad.

Kirim Alivi, Mjumbe wa Kamisheni ya Usalama na Ulinzi katika Bunge la Iraq

Katika siku za hivi karibuni, magaidi wa kundi la Daesh (ISIS) walifanya mashambulizi katika vijiji viwili vya mkoa wa Kirkuk na kituo kimoja cha jeshi la serikali katika jimbo la Diyala. Kwa sasa raia, makundi ya kisiasa na akthari ya viongozi wa Iraq akiwemo Mustafa Al-Kadhimi, Waziri Mkuu Mpya wa nchi hiyo wanafuatilia suala la kutimuliwa askari vamizi wa Marekani katika nchi hiyo ya Kiarabu.