-
Vikwazo vipya vya Marekani dhidi ya Iran; muendelezo wa sera za mashinikizo ya juu kabisa
Jan 11, 2020 04:43Katika zama za utawala wa Rais Donald Trump, serikali ya Marekani imekuwa ikifuatilia sera za mashinikizo ya juu kabisa dhidi ya Iran na katika fremu hiyo mnamo Mei 8 2018, Washington ilitangaza kujiondoa katika mapatano ya nyuklia ya JCPOA na baada ya hapo ikaweka vikwazo shadidi zaidi dhidi ya Iran. Pamoja na kuwa vikwazo hivyo havijafikia malengo yaliyokusudiwa, Marekani inasisitiza kuendeleza sera yake ya kushadidisha vikwazo.
-
Amir Hatami: Marekani inapaswa kuhitimisha haraka uvamizi wake Asia Magharibi
Jan 11, 2020 01:20Waziri wa Ulinzi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, ili kukabiliana na mizozo na uzushaji wa migogoro na ukosefu wa amani katika eneo la Asia Magharibi, kuna ulazima wa uvamizi na uangiliaji wa Marekani katika masuala ya ndani ya eneo hili kuhitimishwa haraka iwezekanavyo.
-
Mashauriano ya kidiplomasia ya Iran kwa ajili ya kuarifisha jinai za Marekani
Jan 10, 2020 07:30Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema katika mazungumzo yake ya simu na viongozi wa nchi kadhaa jirani, nchi za Ulaya na Afrika kwamba Iran inaunga mkono amani na usalama lakini haitakaa kimya mbele ya vitimbi vya Marekani.
-
Umati mkubwa wa Wairaqi wakusanyika mahali walipouawa shahidi Qassem Soleimani na Abu Mahdi al-Muhandis
Jan 10, 2020 04:41Mamia ya Wairaqi wamekusanyika mahali makombora ya jeshi la kigaidi la Marekani yalipoulenga msafara wa magari yaliyokuwa yamewabeba Luteni Jenerali Qassem Soleimani, Kamanda wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu na Abu Mahdi al-Muhandis, Naibu Mkuu wa Jeshi la Kujitolea la Wananchi wa Iraq la Al-hashdu-Sha'abi na kulaani jinai hiyo ya Marekani.
-
Majibu ya kutapatapa ya Trump baada ya Iran kupiga kwa makombora kambi za Marekani + Video
Jan 09, 2020 07:20Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imetekeleza kivitendo ahadi yake ya kutoa jibu kali kwa jinai ya Marekani ya kumuua kigaidi Luteni Jenerali Qassem Soleimani, Kamanda Mkuu wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu SEPAH.
-
Onyo kali la Muqtada al-Sadr na kuwa pamoja makundi yote ya muqawama nchini Iraq dhidi ya Marekani
Jan 08, 2020 21:45Moja ya matokeo muhimu ya jinai ya serikali ya kigaidi ya Marekani ya kumuua shahidi Luteni Jenerali Qassim Soleimani na Abu Mahdi al-Mohandes na watu wanane waliokuwa wamefuatana nao ni kujitokeza hali ya umoja baina ya makundi ya muqawama nchini Iraq dhidi ya Marekani.
-
Zaidi ya magaidi 80 wa Kimarekani waangamizwa katika shambulio la SEPAH
Jan 08, 2020 09:38Afisa mmoja mwandamizi wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu SEPAH amesema kuwa, zaidi ya magaidi 80 wa jeshi la Marekani wameangamizwa na karibu 200 wengine wamejeruhiwa katika majibu makali yaliyotolewa na Iran dhidi ya kambi mbili za kijeshi za nchi hiyo huko Iraq.
-
Rouhani: Majibu kamili ya Iran ni kukatwa miguu ya Wamarekani Asia Magharibi
Jan 08, 2020 08:03Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amegusia majibu makali yaliyotolewa usiku wa kuamkia leo na Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu SEPAH ya kuwashambulia magaidi wa Kimarekani katika kambi zao mbili za kijeshi nchini Iraq na kusema kuwa, majibu kamili ya Iran kwa jinai za Wamarekani ni kukatwa miguu yao kwenye eneo hili.
-
Kiongozi Muadhamu: Iran imejizatiti mkabala wa madola ya kibeberu
Jan 08, 2020 04:49Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema taifa la Iran limejiandaa na kujizatiti barabara mkabala wa madola ya kibeberu duniani.
-
Meja Jenerali Baqeri: Tutatoa jibu kali zaidi kwa hatua yoyote ovu ya US
Jan 08, 2020 04:34Mkuu wa Vikosi vya Ulinzi vya Iran amesema kuwa, majeshi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran yatatoa jibu kali zaidi na kwa nguvu zote dhidi ya hatua yoyote ghalati na ovu ya Marekani.