Zaidi ya magaidi 80 wa Kimarekani waangamizwa katika shambulio la SEPAH
Afisa mmoja mwandamizi wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu SEPAH amesema kuwa, zaidi ya magaidi 80 wa jeshi la Marekani wameangamizwa na karibu 200 wengine wamejeruhiwa katika majibu makali yaliyotolewa na Iran dhidi ya kambi mbili za kijeshi za nchi hiyo huko Iraq.
Afisa huyo mwandamizi wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Kiislamu SEPAH amesema hayo katika mahojiano aliyofanyiwa na shirika la habari la FARS na kuongeza kuwa, kwa mujibu wa ripoti za kina na za kuaminika, helikopta za Marekani zimefanya haraka kuondoa majeruhi na wanajeshi wake waliouawa katika kambi ya kijeshi ya Ain al Asad huko al Anbar, Iraq.
Kabla ya hapo duru za kuaminika zilikuwa zimesema kuwa, wanajeshi wa Marekani wamewaondoa haraka majeruhi na wanajeshi wao waliouawa ikiwa ni njama ya kupotosha walimwengu na kupunguza idadi ya hasara walizopata.
Afisa huyo mwandamizi wa jeshi la SEPAH ameongeza kuwa, kambi ya kijeshi la Ain al Asad ilikuwa ni eneo muhimu la kiistratijia kwa jeshi la Marekani na kwamba helikopta na ndege nyingi zisizo na rubani (droni) za Marekani zilikuwepo kwenye kambi hiyo.

Ameongeza kuwa, maeneo 20 muhimu sana ya kambi hiyo yamepigwa na makombora ya Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu SEPAH na droni nyingi za jeshi la kigaidi la Marekani zimeteketezwa kwenye shambulio hilo la kulipiza kisasi.
Ripoti hiyo imeongeza kuwa, hakuna kombora hata moja la Iran lililotunguliwa na mfumo wa kujilinda na makombora wa Marekani kwenye eneo hilo na kwamba makombora yote yamepiga shabaha kwa ustadi mkubwa.
Vile vile amesema, Iran imeainisha maeneo 104 muhimu mno ya Marekani katika eneo hili ambayo yatashambuliwa mara moja iwapo Washington itafanya uchokozi mwingine wowote.