Amir Hatami: Marekani inapaswa kuhitimisha haraka uvamizi wake Asia Magharibi
Waziri wa Ulinzi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, ili kukabiliana na mizozo na uzushaji wa migogoro na ukosefu wa amani katika eneo la Asia Magharibi, kuna ulazima wa uvamizi na uangiliaji wa Marekani katika masuala ya ndani ya eneo hili kuhitimishwa haraka iwezekanavyo.
Brigedia Jenerali Amir Hatami amesema hayo katika mazungumzo yake kwa njia ya simu na Taro Kono, Waziri wa Ulinzi wa Japan na kueleza kwamba, kuuawa na Marekani Luteni Jenerali Qassim, Kamanda wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) huko nchini Iraq ni jinai kubwa ambayo haijawahi kushuhudiwa.
Waziri wa Ulinzi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ameongeza kuwa, kwa mujibu azimio lililo wazi la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa hatua hiyo ya Marekani ni mfano wa wazi kabisa wa ugaidi wa kiserikali.

Brigedia Jenerali Amir Hatami ameashiria kulaaniwa hatua hiyo ya Marekani na mataifa yote huru duniani na kueleza kwamba, sababu ya mizozo na migogoro katika eneo la Asia Magharibi na kuweko Marekani katika eneo hili.
Kwa upande wake Taro Kono, Waziri wa Ulinzi wa Japan amesema kuwa, nchi yake iko tayari kusaidia juhudi zozote zenye lengo la kupunguza mizozo na mivutano katika eneo.
Kadhalika Waziri wa Ulinzi wa Japan amesisitiza kuwa, nchi yake haitashiriki katika miungano ya kijeshi inayoongozwa na Marekani katika eneo hili.