-
Maulamaa wa Lebanon watangaza mshikamamo wao kwa Iran mkabala na vikwazo vya Marekani
Aug 15, 2018 10:32Maulama wa kidini wa nchini Lebanon wamelaani mashinikizo na vikwazo vya Marekani dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na kusisitiza kuwa wanaiunga mkono kikamilifu Tehran.
-
Radiamali mbalimbali kwa madai ya haki za binadamu ya Marekani
Aug 15, 2018 06:41Naibu Katibu Mkuu wa harakati ya Hizbullah ya Lebanon ameashiria urongo wa madai ya Marekani kuhusiana na haki za binadamu na kusisitiza kuwa, watu wote ulimwenguni wanapaswa kutambua kuwa, Marekani ni dola laghai na haipasi kuamini hata kidogo siasa za Washington.
-
Uturuki yajibu mapigo, yaziwekea vikwazo bidhaa za kielektroniki za Marekani
Aug 14, 2018 22:05Rais Recep Tayyip Erdoğan wa Uturuki ametangaza kuwekewa vikwazo bidhaa za kielektroniki zinazozalishwa nchini Marekani.
-
Kiongozi Muadhamu: Hatutafanya mazungumzo na Marekani
Aug 13, 2018 10:36Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ameashiria matamashi na lugha zisizo na adabu za viongozi wa Marekani kuhusiana na vikwazo, vita na mazungumzo na Iran kusema kuwa, tunasisitiza kwamba, hakutatokea vita na hatutafanya mazungumzo.
-
Wakristo wa Iran wamwambia Pompeo: Wafuasi wa dini za wachache Iran hawahitajii usimamizi wa Marekani
Aug 12, 2018 22:21Jumuiya ya Wakristo wa Assyrian nchini Iran imejibu ujumbe wa Twitter wa Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Marekani aliyedai kuwa wafuasi wa dini za waliowachache wanasumbuliwa na kunyimwa haki zao za binadamu hapa nchini kwa kusema kuwa: Wafuasi wa dini za waliowachache nchini Iran hawahitaji usimamizi wa Marekani.
-
Onyo la Uturuki kwa Marekani kufuatia hatua ya Washington kuzipandishia ushuru wa forodha bidhaa za Uturuki
Aug 12, 2018 07:12Wizara ya Mambo ya Nje ya Uturuki imetoa taarifa ikisisitiza kuchukua hatua za ulipizaji kisasi kufuatia kitendo cha Marekani cha kuzipandishia ushuru wa forodha bidhaa za chuma na aluminiamu za nchi hiyo.
-
Indhari ya Shirika la Kimataifa la Nishati kuhusu kuiwekea vikwazo vya mafuta Iran
Aug 12, 2018 02:45Rais Donald Trump wa Marekani tarehe Nane Mei mwaka huu alikariri madai yasiyo na msingi dhidi ya Iran na kutangaza kujitoa Marekani katika makubaliano ya nyuklia ya JCPOA na kuvirejesha vikwazo vya nyuklia katika muda wa miezi mitatu hadi sita ijayo. Duru ya kwanza ya vikwazo vya Marekani dhidi ya Iran imeanza kutekelezwa tangu tarehe 7 mwezi huu wa Agosti; hatua iliyolaaniwa vikali kimataifa.
-
Magazeti 70 Marekani yachukua msimamo wa kukabiliana na hujuma za Trump dhidi ya vyombo vya habari
Aug 12, 2018 02:45Katika hatua ambayo haijawahi kushuhudiwa katika historia ya Marekani, gazeti moja la nchi hiyo limetoa wito wa kuchukuliwa hatua ya pamoja na magazeti yote ya nchi hiyo kukabiliana na kitendo cha rais Donald Trump cha kutoa kauli chafu mtawalia kuvishambulia vyombo vya habari.
-
Zarif: Hakuna mazungumzo baina ya Iran na Marekani, mkutano wa New York
Aug 11, 2018 22:05Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amekanusha ripoti za vyombo vya habari kuhusu uwezekano wa kufanyika mazungumzo baina ya maafisa wa Iran na Marekani kandokando ya mkutano ujao wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa mjini New York.
-
Russia: Marekani inaweka vikwazo dhidi ya nchi nyingine ili kutatua matatizo yake ya kifedha
Aug 11, 2018 22:04Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Russia amesema kuwa, Marekani inaziwekea vikwazo vya upande mmoja nchi nyingine kwa shabaha ya kuondoa matatizo yake ya kifedha na kuziba nakisi ya mapato yake.