-
Mahakama ya Rufaa Misri yaafiki kifungo cha maisha jela kwa viongozi 11 wa Ikhwani
Jul 11, 2021 21:56Mahakama ya Rufaa ya Misri imeidhinisha kifungo cha maisha jela kwa viongozi 11 wa Harakati ya Ikhwanul Muslimin.
-
Ombi la Misri na Sudan kwa Baraza la Usalama; mgogoro wa Bwawa la An Nahda
Jun 28, 2021 05:56Huku awamu ya pili ya kujazwa maji katika Bwawa la An Nahda (Grand Renaissance Dam-GERD-) la Ethiopia katika Mto Nile ikikaribia, Misri na Sudan, nchi mbili ambazo zinapinga ujenzi wa bwawa hilo, zimetaka ujazwaji maji huo usitishwe kwa muda. Nchi hizo mbili zimetaka Ethiopia izipatie dhamana kuwa haki zao zitalindwa, jambo ambalo limeibua taharuki mpya baina ya nchi hizo tatu.
-
Ayman Nour: Kunyongwa viongozi wa Ikhwani kutazusha machafuko nchini Misri
Jun 26, 2021 21:57Kiongozi wa chama cha El Ghad nchini Misri ameitaka Kamati ya Kimataifa ya Kuzuia Adhabu ya Kifo katika nchi za Kiarabu kuwasiliana na jumuiya za kimataifa kwa ajili ya kusitisha utekelezaji wa hukumu ya kifo iliyotolewa dhidi ya viongozi kadhaa wa chama cha Ikhwanul Muslimin.
-
Watu 30 wapoteza maisha na kujeruhiwa katika ajali ya treni na basi kusini mwa Cairo
Jun 21, 2021 22:39Watu wanne wameaga dunia na 26 wamejeruhiwa katika ajali ya jana usiku iliyozihusisha treni ya mizigo na basi lililokuwa limebeba wafanyakazi huko kusini mwa Cairo, mji mkuu wa Misri.
-
Jukwaa la Waarabu lazitaka jumuiya za kimataifa zisitishe kunyongwa Wamisri 12, wamo viongozi wa Ikhwani
Jun 17, 2021 02:41Jukwaa la Warabu limeziomba jumuiya na mashirika ya kimataifa ya kutetea haki za binadamu kuingilia kati na kusitisha utekelezaji wa hukumu ya kifo ya Wamisri 12 wakiwemo viongozi waandamizii wa harakati ya upinzani ya Ikhwanul Muslimin.
-
Abiy Ahmed: Bwawa la Renaissance litazifaidisha pia Sudan na Misri
Jun 07, 2021 08:22Waziri Mkuu wa Ethiopia amesema kuwa ujenzi wa Bwawa la Renaissance utakuwa na faida si kwa nchi hiyo pekee bali pia kwa nchi za Misri na Ethiopia.
-
Misri yauonya utawala wa Kizayuni wa Israel kuhusu Ukanda wa Ghaza
May 31, 2021 02:52Waziri wa Mambo ya Nje wa Misri, usiku wa kuamkia leo ameuonya utawala wa Kizayuni wa Israel kuhusu hatari za kuvunja makubaliano ya kusimamisha vita ya Ghaza.
-
Maafisa usalama wa Misri wawasili katika Ukanda wa Ghaza, Palestina
May 29, 2021 05:10Duru za habari zimetangaza kuwa ujumbe maalumu wa maafisa usalama wa Misri umewasili katika Ukanda wa Ghaza huko Palestina kwa ajili ya kufanya mazungumzo na wakuu wa makundi ya muqawama.
-
Misri yawanyonga watuhumiwa wa uvamizi dhidi ya kituo cha polisi, Amnesty yalaani
Apr 27, 2021 02:15Idara ya Magereza ya Misri inayoongozwa na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi hiyo imetangaza kuwa, imetekeleza hukumu ya kifo dhidi ya watu 9 waliohukumiwa kwa hatia ya kile kinachotajwa kuwa ni uvamizi dhidi ya kituo cha polisi.
-
Ajali ya tatu ya treni Misri katika chini ya mwezi mmoja, mkuu wa Shirika la Reli ajiuzulu
Apr 19, 2021 06:11Mkuu wa Shirika la Reli la Misri amejiuzulu baada ya kutokea ajali ya tatu ya treni nchini humo katika kipindi cha chini ya mwezi mmoja.